Naomba Ushauri, nimefilisika baada ya kuoa!

Naomba Ushauri, nimefilisika baada ya kuoa!

Je, upi uamuzi wako kwenye ndoa?

  • Total voters
    53
Kwa mwaka zimekatika 7Million inamaana kwamba mimi napeleka hela chooni wenzangu ambao hawajaoa wanapeleka hela kwenye ujenzi na kupanua biashara zao
Bado kidogo maana kula hakukwepeki yani maisha lazima yaendelee. We pbana kuongeza kipato. Milion saba kwa mwaka ni kama 550000 kwa mwezi so kama hiyo inajumuisha chakula na kodi na mengine si nyingi mkuu. Je, ukiweka mtoto na mtoto awe anasoma shule za saint mzungu si utakodisha gari la PA ulalamike mtaa mzma?
 
kweli wanaume wanazid kupungua kwa kasi duniani..
.
uanaume sio kufungua zipu kaka uanaume kamili ni kuwa kuna watu wako nyuma yako wanaokuangali yaani pasipo wewe mambo yao na yako hayaendi kabsa...
 
Kuna wanawake wengine hawana baraka, hawana muunganiko kabisa na kinyume chake ni kweli
Bora umeandika hii comment. Kama hata akiwa girlfriend tu ukawa hupati riziki au mambo hayaeleweki piga tu chini. Wanawake wengine wana nuksi tu. Lakini jamaa akae chini na mke wake washauriane kuhusu bajeti. Utakuta manzi hapo anajipigia hela kupitia tu hayo matumizi ya kila siku.
 
Kaka pole sana kwa changamoto, kikubwa ni kujipanga vzur tu utaona mambo yatavyojipa. Mimi binafsi nilikuwa naishi dar nilikuwa nmeoa pia kipindi kile nilikuwa nalipwa laki tatu nalipa kodi na mambo mengine yanaendelea ila kwa sasa nipo mkoani nasongesha maisha. Ushauri wangu tafuta chumba/ nyumba ambayo utaweza kuimudu kulipa kodi alafu utaona mambo yatavyoenda.
 
Yaan mimi ni kinyume na ww, kabla sijaoa nlikuwa sina hela, hazikai mfukon lln now nimeoa si haba, bidada anaingiza hela, kwa siku sikosi hela ya petrol,

Aisee Tunatofutiana katika maisha, yaan wkt ww unalalamika kuna watu tuna enjoy sana aisee, pole mkuu hilo ndilo fungu lako usibadili mke suo nguo hiyo, Mungu atakusaidia tu atabalilika
 
Kabla sijaoa nilikua na maisha mazuri sana, hela ilikuwa inakaa mfukoni, laki tatu inakaa hata miezi mitatu kwenye chakula, sikuwa mtu wa mawazo ya usumbufu wa kudaiwa daiwa vitu vya ndani kifupi nilikuwa naenjoy sana maisha yale hasa kwenye mambo ya kiuchumi yani sikuwa nakosa hela mfukoni.

Baada ya kuoa mwaka jana mwezi wa saba hali ikabadilika ghafla hela zikawa zinaishia kwenye chakula, mimi kama mwanaume naweza kununua hata maandazi matano nikanywa na juice na siku ikaisha ila kwa mke hutaweza kufanya hivyo itabidi utoe hela ya chakula na kwa maisha ya Dar sio chini ya elfu 10 kwa siku yaani kwa watu wawili mme na mke ukiwa na mtoto inaeza fikia mpka 20 kwa siku.

Kwahiyo kwa siku lazima 10 initoke kwa wiki elfu 70 mwezi 280,000, Mwaka 3,360,000. Hapo bado sijaweka umeme, maji, vocha, nauli za kwenda sokoni na kwenye mishe zangu na matibabu pia, bado kodi ambayo kwa mwezi nalipa 100,000. Kwahiyo chakula na kodi kwa mwaka ni 4,560,000 bado sijaweka vingine kwahiyo kwa mwaka ikanigharimu zaidi ya million 7.

Hapa nilipo hali imekuwa mbaya hasa njaa, hela zangu zimeisha kwasababu ya kuoa tu kwasababu tu ya kutaka kumiliki mbunye wakati sabuni zipo na oil na mimi sio mlevi wala mtu wa kuhonga.

Nimegundua kuwa kuoa ni hasara kubwa sana duniani sasa naomba ushauri nirudishe huyu mke ili niepuke hizi hasara ama nibaki nae kwasababu yakutaka kuwa na mbunye karibu nife maskini mwishowe.

Kama Diamond Platnumz mke amemshinda akaacha, Alikiba akaacha, Bill Gates kaacha mimi nitaweza vipi kuishi na mke ikiwa matajiri yamewashinda?
Umeanza vizuri ila umevuruga hapo kati na mwishoni.

Acha utoto.
 
Kama huna mtaji fanya kazi ngumu ngumu ndio zenye hela wale wanaoendesha maguta ya baiskeli mjini sio wajinga wanaingiza hadi elfu 30 kwa siku sasa wewe unaoa slay queen ambaye hajishughulishi na kitu unafanya kazi za viwandani salary laki mbili muda wakuoa bado sana jipange
 
Kabla sijaoa nilikua na maisha mazuri sana, hela ilikuwa inakaa mfukoni, laki tatu inakaa hata miezi mitatu kwenye chakula, sikuwa mtu wa mawazo ya usumbufu wa kudaiwa daiwa vitu vya ndani kifupi nilikuwa naenjoy sana maisha yale hasa kwenye mambo ya kiuchumi yani sikuwa nakosa hela mfukoni.

Baada ya kuoa mwaka jana mwezi wa saba hali ikabadilika ghafla hela zikawa zinaishia kwenye chakula, mimi kama mwanaume naweza kununua hata maandazi matano nikanywa na juice na siku ikaisha ila kwa mke hutaweza kufanya hivyo itabidi utoe hela ya chakula na kwa maisha ya Dar sio chini ya elfu 10 kwa siku yaani kwa watu wawili mme na mke ukiwa na mtoto inaeza fikia mpka 20 kwa siku.

Kwahiyo kwa siku lazima 10 initoke kwa wiki elfu 70 mwezi 280,000, Mwaka 3,360,000. Hapo bado sijaweka umeme, maji, vocha, nauli za kwenda sokoni na kwenye mishe zangu na matibabu pia, bado kodi ambayo kwa mwezi nalipa 100,000. Kwahiyo chakula na kodi kwa mwaka ni 4,560,000 bado sijaweka vingine kwahiyo kwa mwaka ikanigharimu zaidi ya million 7.

Hapa nilipo hali imekuwa mbaya hasa njaa, hela zangu zimeisha kwasababu ya kuoa tu kwasababu tu ya kutaka kumiliki mbunye wakati sabuni zipo na oil na mimi sio mlevi wala mtu wa kuhonga.

Nimegundua kuwa kuoa ni hasara kubwa sana duniani sasa naomba ushauri nirudishe huyu mke ili niepuke hizi hasara ama nibaki nae kwasababu yakutaka kuwa na mbunye karibu nife maskini mwishowe.

Kama Diamond Platnumz mke amemshinda akaacha, Alikiba akaacha, Bill Gates kaacha mimi nitaweza vipi kuishi na mke ikiwa matajiri yamewashinda?
Kwahiyo unamtafutia sababu ya kumuacha ili uishi na sabuni + oil?🤔
 
Acha tu ndugu yangu ni mateso makubwa sana kwa mwaka inakatika 7M tayari hapo ningekuwa na kiwanga changu jamani😭
Huo mwaka mzima ungekuwa hutumii pesa za chakula wala kulipa kodi? Au ungekuwa unapata constipation kila siku kwa kushindia maandazi 5 na juice?

Kuoa maana yake ni kukubali majukumu kuwa upo tayari kumvisha,kumlisha na kumlaza mkeo sehemu nzuri na vile vile kuwa tayari kuhudumia kiumbe kitakachokuja kutoka katika uti wa mgongo wako!

Vilevile jua huyo mke na mtoto wanapokuwa chini yako nao huwa na riziki zao ambazo Mungu huzipitisha kupitia wewe.

Ndoa ni baraka na ni heshima kwa mwanaume. Mwanaume kunung'unika pesa unayoitumia kwa ajili ya familia yako ni uzwazwa wa kiwango cha SGR.
 
Back
Top Bottom