Naomba Ushauri: Nimepata Kesi baada ya kumpiga mvuta sigara

Naomba Ushauri: Nimepata Kesi baada ya kumpiga mvuta sigara

wavuta sigara wanaamini kila mtu anapenda sigara. Huwa sipendi kabisaa hiyo harufu.
Nimekaa kwenye benchi kijiweni nashangaa ghafla mtu kawasha kiberiti puuff. Naangalia pembeni pua yangu inanakutana na mosh...
Umeshasema ni mzee wa makamo, ulipata ujasiri gani kumpiga?

Unajua kesi nyingine nizakujitakia; kwanini usingemwambia tu au ukajiondokea zako kuepusha shari?

Mimi sijui kifungu cha kukusaidia kwa kweli kwani naona tayari una kosa la kupiga tena Mzee....
 
Moja tambua police sio mahakamani ata kama upo sahihi police hawawezi kukuachia wao ni kukuweka ndani, chukua maelezo upate dhamana kisha hatua za mahakamani zitafuata.

Hata ukiwa mjuaji sijui sijampiga au kavuta sigara hiyo sio jukumu la polisi kutaka mashahidi.
Mlalamikaji atakushtaki kwa kosa la kumshambulia na kumjeruhi mahakama imishaamua na kutoa hukumu.
Wewe kama una kesi au malalamiko yako utayapeleka mahakamani kesi itangurumishwa kwa miezi kdhaa kisha utapeleka mashahidi na mlalamikiwa ataleta wa kwake hukumu itatolewa

Police sio sehemu ya kujitetea ni kutoa maelezo tu. Mengine ni mbwembwe sijui kuandikishana deni sio kazi ya police kutoa suluhishi za kesi basi tu wanajikutaga mahakimu.
Kama wewe ni mtumishi wa uma unaweza kutumia kitambulisho chako cha kazi kujiwekea mdhamana huitaji mdhamini mengine utayajua mbele ya safari. Kesi ni kesi ni usumbufu kama vipi wachenge tu pilice na wasikupate.

Kesi ni ujinga unaweza kupambana mahakamani miezi 4 ukaona mambo yanakuangukia ukajikuta unatoa laki 3 kwa hakimu unapewa kifungo cha nje cha mwaka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Sheria ni kama mchezo tu unapanda, shuka, punda, katisha, juu chini mwisho huujui [emoji1][emoji1]
 
Kijiweni Siyo level yako mkuu, next time utakuja kumwagiwa kahawa ya moto,. Sasa jichanganye ,mahakamani ukamwambie hakimu eti " tulikuwa tumekaa kijiweni mzee akawasha sigara nikampigia"
 
Aliyewahi polisi atahesabika ana haki kwanza halafu huko mbeleni utaenda kujielezea kwanini ulimchapa. Kuna sababu gani ya kumchapa?

Angekufia hapo?

Unajua afya yake?

Stress za maisha zisikupeleke mbio hivo mzee
 
Hongera mkuu kwa kuifunza adabu hiyo taka taka. Ipo sheria inayokataza kuvuta sigara kwenye umma Adhabu yake nadhani ni Mil 2 au kifungo miezi sita kesho nitaiweka hapa jamvini.
Na walipa Kodi wakubwa ni wavuta sigara
 
We kalale selo chati ya mwisho mwisho kabla ujakabidhi simu kaunta.
Andaa wadhamini kesho
 
wavuta sigara wanaamini kila mtu anapenda sigara. Huwa sipendi kabisaa hiyo harufu.
Nimekaa kwenye benchi kijiweni nashangaa ghafla mtu kawasha kiberiti puuff...
We jamaa umeshindwa ata kuinuka hapo mengine yanakwepeka
 
Nakereka na wavuta sigara na walevi.
Yaani nikiwaona wana matatizo nafurahi sana, ni sawa na mlevi akipata ajali natamani nimuumize mara ya pili
 
Back
Top Bottom