Mimi na mpenzi wangu tuliyeishi pamoja kwa zaidi ya miaka miwili tuliachana baada ya mwanamke huyo kuanza visa na akaenda nyumbani kwao. Badae akaibukia mahakamani akiomba talaka na mgawanyo wa mali akiongozwa na wakili mmoja hivi ambae ni ndugu yake.
Moja ya mali ni nyumba ambayo mahakama imeona tumechuma pamoja lakini mahakama hiyohiyo amejiridhisha kuwa kiwanja ni mali yangu peke yangu. Sasa mahakama imeagiza nyumba iuzwe tugawane kwa asilimia ambazo mahakama imeziona. Mimi sitaki kuuza kiwanja changu ambacho mahakama pia imedhibitisha kuwa ni mali yangu pekee yangu ila nyumba ambayo imejengwa ndio imeonekana tumechangia kujenga na huyo mwanamke.
Je hii hukumu itatekelezeka vipi kisheria maana ndio tunasubili uthamini?
Ushauri wangu
1. Anatakiwa mtu adhaminishe bei ya hiyo nyumba kwa sasa pamoja na kiwanja
2. Halafu adhanishe bei ya hicho kiwanja chenyewe kwa sasa
3. Chukua bei ya Nyumba toa kiwanja gawanya kwa mbili
Mfano bei ya nyumba pamoja na kiwanja shs 45,000,000
Bei ya kiwanja kwa sasa; shs 15,000,000
Unachukua bei ya nyumba shs. 45,000,000 toa shs 15,000,000 ya kiwanja = shs 30,000,000.
Ili kugawana sawa; chukua shs 30,000,000 gawanya kwa mbili = shs 15,000,000.
Kama hutaki kuuza nyumba; wewe mtafutie shs 15,000,000 ambayo ndio mgao wake.
Sina hakika kama ni kisheria ila naona hivyo utakuwa umemtendea haki