Naomba ushauri, nimepewa hukumu ya kugawana mali na aliyekuwa mke wangu

Tafauta mthamini apige thamani ya nyumba (Bila kiwanja), then mrudishie hela yake (mgao wake). Halafu nyumba inabaki kuwa yako.
 
Tafuta mteja wa bei rahisi Mfano 10m, kama hana uchungu na nyumba nia ni kukomoa atakubali, mpe m5 ila mteja ni wewe mwenyewe.
 
Diamond platnumz angekuwa anawapa wapenzi mali wakiachana asingebaki na kitu
 
Mimi nadhan hapo kwakuwa huyo mwanamke anataka kukukomoa, baai nawewe mkomoe.
Iambie Mahakama kuwa wewe kiwanja chako huna mpango wa kukiuza,
Na kuhusu nyumba ikiwa mtagawana kwa vyumba au thamani ya nyumba, basi mgao ukishapita wa nyumba mwambie kuwa aiondoe upande wake kwenye kiwanja chako. OVA
 
Kudadeq...Mwanamke alikua ni genius......sema akakutana na Albert Einstein [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ndo Ile mnaishi Kwa kuliana timing

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 

Ushauri wangu
1. Anatakiwa mtu adhaminishe bei ya hiyo nyumba kwa sasa pamoja na kiwanja
2. Halafu adhanishe bei ya hicho kiwanja chenyewe kwa sasa
3. Chukua bei ya Nyumba toa kiwanja gawanya kwa mbili

Mfano bei ya nyumba pamoja na kiwanja shs 45,000,000
Bei ya kiwanja kwa sasa; shs 15,000,000
Unachukua bei ya nyumba shs. 45,000,000 toa shs 15,000,000 ya kiwanja = shs 30,000,000.
Ili kugawana sawa; chukua shs 30,000,000 gawanya kwa mbili = shs 15,000,000.
Kama hutaki kuuza nyumba; wewe mtafutie shs 15,000,000 ambayo ndio mgao wake.

Sina hakika kama ni kisheria ila naona hivyo utakuwa umemtendea haki
 
Ndio hukumu itatekelezeka vizuri kabisa. Hicho unachofikiria nijanja ya nyani.
Nikujuze TU kwamba mgawanyo wa mali huangalia mchango wa Kila upande katika kupatika au kuendelezwa Kwa mali husika. Nikweli alikukuta na kiwanja lakini kiwanja kimeendelezwa baada ya wewe kuanza kuishinae na bilashaka amethibitisha mchangowake katika kukiendeleza ndio maana amepata sehemu ya asilimia.

njia yakujinasua, mlipe asilimia zake ili wewe ubaki na umiliki kamili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…