Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Kwanini mlivyopata habari jamaa kaoa hamkuwaambia wahusika ili wasitishe safari? Wewe na ukoo wako mnatabia mbaya
Kweli hasira hasara.waliomshauri akaekimnya basi wamshauri pia aombe msamaha
 
Achana nae huyu? Yaan unasikia rumours alaf unaamua kwa hasira....HAFAI KUOLEWA KABISA ,MWANAMMKE WA NAMNA HIII BUREEEE KABISA HAFAI HATA KUOELEWA NA SHETANI......ajioe mwenyewe
 
I hate to say this"KAMA NI WANYAKYUSA SAHAU KUHUSU NDOA NA HUYU MTOTO WAO NA HATA KAMA MTAFOSI UKOO MZIMA UTAKUA HAUKUPENDI."
 
Kwa Ufupi endelea na maishaa yako tu yaliyotojekea yametokeaa toka mwanzo Mama alipoziraa na kususia ndoa yako Iliingia Dosari Kubwa sana na kimsingi ilivunjika kabla haya ya kufungwaa so kilichotokea sio kwa akili yako au ni kosa lako noo hii ndo haikutakiwa kufungwa. Umemuumiza sana kaka wa watu kwa kusikiliza maneno lakini umeumiza ndugu zake pia na kumchafua sana msameane maisha yaendeler mbele.


Next time usimhukumu mtu kwa maneno ya kuambiwaa hata siku mojaaa...!! HUFAI KUWA MKE.
 
Hii story itakuwa ya kutunga. Upo kwenye relationship na karibu unafunga ndoa hujafanya due diligence? Unampenda kweli au unatafuta unafuu wa maisha? Jamaa is smart . Wewe kupata mme itakuwa kazi considering your status . Hivi unafanya shughuli gani?
 
Hufai hata kushauriwa,
 
Wakuu mfikilie nje ya box, Hapo mi naona mchawi wake ni mamaake. Mama yake ndo hataki mwanae aolewe ukute mamaake aliwaambia kakazake wazushe habari za huyo mwamba ana mke maana alionekana kutopendezwa kuwepo kwa iyo ndoa.
Kwani shida iko wapi Kama muoaji anamsomesha mtoto Sema tu hataki kwao wajue, shida ingekuwepo mama mtu kukataa ndoa kisa Kama muoaji anafichwa anaoa singo maza.
 
Pole sana na ninajua huyo mjomba wako unamlaumu sana na baba zako walikuwa sawa maana walitaka kumuenzi baba yako ambaye kwa maelezo yako hayupo hivyo walitaka kumaliza majukumu ya kaka yao..
Sijamlaum
 
Sidhani kama Kosa moja Laweza sababisha nayo?
 
Nimeshaomba msamaha Sana kwa kikichotokea
 
Hii story itakuwa ya kutunga. Upo kwenye relationship na karibu unafunga ndoa hujafanya due diligence? Unampenda kweli au unatafuta unafuu wa maisha? Jamaa is smart . Wewe kupata mme itakuwa kazi considering your status . Hivi unafanya shughuli gani?
This Is the real story japo sijataja mikoa husika nimetumia tafsida, na ukweli imeniuma
 
Hakuna msamaha hapo watu watoke Mbeya hadi Ngara wamepoteza muda na pesa nyingi halafu ati mtu kazima simu niseme ukweli
1. Mna roho mbaya isiyothamini utu
2. Mna tabia mbaya hata kama mtu hamuongei
naye lakini kama kaja kwako inabidi umpokee
vizuri na kumueleze kilichowakwaza vinginevyo
mngepiga simu mapema kuwazuia wasije
3. Hamjitambui wote wewe na hao wazee wako

Hakuna sababu ya kuunga ukoo na ukoo wenye sifa hiizo hapo juu. Siwajui hao mliowatenda lakini nimeumia sana. Ushauri wangu tafuta wa huko huko kwenu Ngara ili akuoe maana mnajuana tabia
 
Utatolewa kafala
 
Mimi Bado nashangaa nasoma na kurudia mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa. Lengo haswa la haya maswala ya Posa,mahari na ndoa hadi kuhusisha watu wazima ni kwasababu ya hekima na busara zao

Sasa wajomba wanajitoa kwenye shughuli katikati bila kuwasiliana na wakubwa wenzao kule, halaf bi harusi anamtumia msg mwenzake yuko kahama kuwa hairisheni safari yaaani haaingii akilini hata kidogo

Kwanini wasingewesubiri mpaka wafike watoe msimamo wao kama familia kila mtu anachukua tym zake(Uzuri kwa hapa ingewapa nafasi ya upande wa pili kujieleza/kujitetea) na kila kitu kingeenda poa.

Mambo matatu nnayoyaona
1: Ndoa yenu imeanza misukosuko kabla hata haijaanza. Mimi nisingekuoa tena hata kama ningekusamehe

2: Wewe na familia yako wote hamna akili,busara wala hekima(am sorry to say namanisha hadi hao wajomba wote)

3: Jamaa hata akikukubali na kukuoa na kukusamehe kwakua ana kupenda. Ndugu zake hawatakusamehe wala kusahau na utakua na ndoa ngumu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…