Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Naomba ushauri nimewakosea sana wanaoenda kuwa wakwe zangu kutokana na mkanganyiko wa familia yangu/Sikutokea siku ya Send off

Dada zetu huwa mnakosaga uwezo wa kufanya uchunguzi kwanza... Hilo tu ndilo linalowaangusha kila mara... Ulipagawa na tiketi ya ndege... Maneno ya mama yalikuchanganya... Tetesi zikakumaliza kabisa... Pole sana
 
Single maza eti anakasirika kuwa mke wa pili, yaani wewe hata ukiolewa kama mke wa nne inabidi ushukuru, wewe ni bidhaa iliyotumika. Ona sasa umepiga teke bakuli la uji kwa ujinga wako, endelea kupiga miayo kistaarabu....hatutaki makelele.

[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Mwanamke mwenzangu umekosea tena umekosea sana, yani ukoo wako wote umekosea. Sawa taarifa mlipata tarehe 8 na wao waliondoka mbeya tarehe 7 kuja ngara, ndugu zako walishindwa nini kuwafata familia ya mchumba wako siku waliofika kwenda kuliongelea hilo jambo kabla ya sherehe?

Hata kam wangefika tarehe 10 hiyo hiyo na hata kama ni kweli ana mke uungwana ilikuwa ni watu wazima kwenda kuongea uso kwa uso na kama walikuwa wameshafanya maamuzi kwamba hawataki tena wewe kuolewa kwenye hiyo familia lilikuwa ni jambo la kuongea na kufikia muafaka shehehe ivunjwe kuliko kuwatelekeza bila taarifa na kuwaaibisha siku ya sherehe. Na nina amini kwamba na mchumba wako pia alikuwa ameshafika ngara, ulipaswa kukutana nae uso kwa uso akupe ukweli wa kilichotokea then ndo ufanya maamuzi, lakini mwenzangu wewe doooh.

The way ambavyo ukoo wenu mzima umeonyesha udhaifu kwenye ku handle hilo jambo kwa upande wangu i think huyo jamaa kuna jambo kaepushwa nalo kutoka kwako aisee what has happened is a blessing in disguise mmejidhalilisha sana. Na unasema jamaa ni mpole na mwenye hekima unahisi anaweza kusamehe ikitokea umeomba msamaha, well, yeye atakusamehe ila familia yake sizani kama itasamehe kirahisi hivyo mana mmewaingiza gharama mwisho mmekuja kuwadhalilisha, kibao kitageuka this time wao ndo watawasusa.

Ushauri wangu kiubinadamu nenda kaombe msamaha, muombe mchumba wako, waombe wazazi wake na ndugu wengine ambao unaweza ku contact nao, na usiombe msamaha kwasababu unataka jamaa akuoa hapana omba msamaha kwa kuwa its the right thing to do.
 
Duh! Una uwezo mdogo wa kufikiri, uwezo mdogo wa kufanya maamuzi, Ni rahisi kuyumbishwa.

Maumivu uliyompa huyoo kijana Ni hatari.

Ivi send-off huwa inaandaliwa upande wa mke au mume? Sijaelewa hapo
 
Yaani kwa akili yako hiyoo komaa tu na Huyo jamaa kama atakuelewa kwa akili hiyohiyo hata hapa JF hawezi kujitokeza mtu wa kukuoa. You are easy to be manipulated yaani unaamua kutokana na tetesi. Yaani mtu aliyeamua kukulinda wewe dhidi ya familia yake wewe unachukulia kirahisi hivyo.
 
Duh! Una uwezo mdogo wa kufikiri, uwezo mdogo wa kufanya maamuzi, Ni rahisi kuyumbishwa.

Maumivu uliyompa huyoo kijana Ni hatari.

Ivi send-off huwa inaandaliwa upande wa mke au mume? Sijaelewa hapo

Hii stori ukiisoma vema unaweza kuhisi ni alkasusi, mara nyingi sendoff na harusi hupishana siku chache tu... hivyo basi ikiwa maandalizi ya sendoff yalikuwa kamili ni wazi kiumeni pia harusi ilikuwa imeiva.

Ila sasa, kwenye stori sijaona ikitajwa kuwa mchumba alishatoka Sauzi manake alipaswa kuhudhuria... pia mwandishi anasema 'hakutokea' kwenye shughuli as if sendoff iliendelea!

Ndugu zake upande wa mke, kama walishajichanga na kusafiri je ilikuwaje reaction yao?

Mwandishi kataja mikoa Mbeya na Ngara, kama ingekuwa kweli kwa tukio hili tungeshasikia!

Baada ya kusema hayo, naomba niiachie mahakama ya JF iamue kuzika au kusafirisha.
 
Mungu amekuepusha na janga kubwa sana huko mbeleni. Achana na huyo mchumba, ndio nimeandika hivyo wala sijakosea kwamba ACHANA
Inaonekana umwkurupuka kuchagua hoja. Jifunze Musoma comments kabla ya kukimbilia kupost.

Baadae ameeleza nijambi gani mama yake hakukubaliana nalo
 
Wewe endelea na maisha yako, nimekuona hufai hata kidogo na huna sifa ya kua mke,kwa nini ulipo sikia jambo la aina hiyo hukuniuliza, unamaansha hata tukianza kuishi watu wakakuletea habari za uongo utaondoka mara moja huna akiri kabisa, halafu unakuja hapa jamvini kuanika upupu wako unazani mm sipo humu jamvini? Umenisababishia hasara kubwa pia umeniaibisha mimi, na familiy yangu mama yangu mpaka amekonda kwa ajili ya ujinga wako, nimeumia sana ila mungu atanipa mke mwema, pia inawezekena mungu kaniepushia jambo hapa,kwenda zako tena sitaki hata kukuona niache niendelee na maisha yangu.
Hahahaha kwa sifa za upole mwanaume aliyemsemea sidhani kama utakuwa ni wewe.
 
Pole , jifunze hasira ni Hasara kabla ya maamuz hakikish unazo Taarfa za kujitoshelezA.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom