Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Sorry kwa ushauri wangu ila ushike huu

Tunajua kila mtu anamheshimu mama, ila kama Mama yako ni bado ni Binti na ana maisha haya ya kisasa, elewa tu kwamba mama ni guberi na haijalishi ni mama alikuzaa, anaweza kua ni wa mjini mjini sana, ila pia kama ni mtu tu anayejiheshimu basi ana mapungufu ya kibinadamu, na kama hiyo nyumba Ina hati za kwako uza sepa, ukifanikiwa huko mbele utakua unamlea Kwa vitu vidogo vidogo
 
Ndugu, kumbuka wadada wa mjini sana na wahuni tu na anaweza akawa mama wa kijana ambaye amemaliza chuo, anaweza kutumia udhaifu wa huyu ni mtoto na kufanya mambo yake ya ajabu ajabu, wapo watoto waliomjengea mama yao na bado mama akaleta mwanaume ambaye hakuzaa nae na Kisha akaanza kumpa huyo mwanaume vile ambavyo walitafuta watoto, mkisikia mama maishani wote ni wamama wenye busara na ni watu wazima hapana
 
Ushauri huu hapa,mia kwa mia
 
Pole sana,ila ukitaka kufanikiwa katika maisha,endelea kumheshimu mama yako.Tafuta namna yoyote
ondoka hapo nyumbani, kama una marafiki uliosoma nao wameishajitegemea kwa kupanga au kujenga waombe
wakufadhili kwa muda uishi nao huku ukiendelea kupambana hata kama ni kazi za zege,Mungu hatakuacha.
 
Japo ipo tofauti kidogo na yako, ila nakumbuka Kuna Mwamba mmoja alikuwa anazinguana na babaake hvyohvyo...uzuri babaake tulikuwa tunapiga nae story, wazee wa mjini, anasema hawezi kuamka Asubuhi anataka kwenda bafuni alafu anapishana na mkwe wake maana jamaa alikuwa anaishi na mke wake hapo kwao, mzee alishajaribu kila njia kumuondoa jamaa nyumbani ila mchizi aligoma, kuna Siku alitoa dirisha jamaa akaweka wavu.Mwisho wa Siku mzee aliwavizia hawapo akabomoa ukuta wa chuma chao...jamaa ikabidi asepe. Huwezi amini jamaa baada kama miezi sita alijenga nyumba yake na alikuwa na project nyngn Kigamboni huko ya nyumba zakupanga ameianza..kiufupi mshkaji baada ya kufukuzwa home alibahatika kupata kazi sehemu ambayo ilikuwa inamuingizia mpunga mrefu sana ukiachana na mshahara wake ambao ulikuwa mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…