Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Huyo ni Mama yako,mueleweshe tu ila hata asipokuelewa wewe mvumilie tu na uondoke hapo home ukapambane ila usimsahau Mama yako wala usimfanye kua ni adui yako,

Kumbuka huyo Mama yeye alikuvumilia mambo mangapi toka ukiwa mchanga mpaka leo hii umekua mtu mzima?

Alivumila mengi sana na kama usemavyo Baba yako alifariki toka wewe ukiwa bado mtoto mchanga,

Achana na fikra za kumkomoa Mama yako,tumia hizo lawama zake kwako kua hasira ya kutafuta hela na sio kumjengea chuki,

Good luck Bro.
Sasa kusaidia akiwa mtoto isiwe kigezo cha kumuumiza mtoto. Hiyo sio sawa.
 
Pole sana mkuu, wakati mwingine wazazi wanazingua sana ikiwa umeshatimiza wajibu wako songa mbele, mama ni mama hata kama ana mapungufu ndio mama huyo, piga kazi na tengeneza pesa, heshima itakuja tu.
Wazazi sio poa mkuu, yaani mimi nakumbuka nilipata tenda kwenye mgodi x na mshahara ulivyokuwa ukitoka nawatumia sometimes hadi mshahara wote, na hao nilio kuwa nawatumia ni babu na bibi maana ndio wamenilea mwisho wa siku tenda iliisha nikarudi kukaa kilicho fata nimasimango balaa.

Nilikuja jisemea kimoyo moyo hapa nianzishe biashara ya chipsi, maana kunakihela nilibaki nacho, nikawa nawasikia wakisema unajifanya unaanzisha biashara? Hutafika popote nakweli bhana mtaji ulikata ndani ya wiki 2, sina ham na wazazi mimi japo huwa nawasaidia na nipo mbali nao nimeajiriwa zangu serikalini.
 
Kuwa makini asije akawa mwanga, anakukalia usitoke kimaisha......machawi ni majitu ya hovyo sana, hakuna cha mzazi wala mtu baki.
Hilo nalo ni neno, maana hawa wazazi wetu bhana alafu nahv unakuwa huna uhakika [emoji1787][emoji1787]
 
Wapo wamama wazazi wenye roho mbaya kama huyo ,

Wengine wanawafukuza Kabisa watoto wao wa kuwazaa.

Pole mwaya,

Muombe Mungu akupe neema akuinue uweze kufanikiwa.
 
Naona umefungua kamlango ka kutiririsha LAANA....! Vyema ufute uzi na uombe msamaha rohoni wa jinsi unavyomuwazia kumtenda vibaya mama..hutakaa ufanikiwe asilani...! Utabak kushika hela ndogo ndogo tu za kula...! Just an advice!.
Laana ipo...
 
Mkuu kama uliweza kufight chuo mpaka ukamjengea mama that means una fighting spirit,kama uliweza kubeba zege then sidhani kama maisha yatakushinda, have confidence,najua saa nyingine maneno ya watu yanaweza yakatupoteza kujiamini na amani,lakini wewe sio mtu wa kukosa kitu... tatizo ukishapata degree unaona mimi sio yule wa kufanya kazi zile tena, Mkuu kwa jinsi maisha yalivyopanda na tatizo la ajira nchini, kazi yoyote ile itakayokuingizia chakula kinywani fanya. Kama wengine walivyoshauri ondoka hapo nyumbani nenda popote, fanya chochote halali kama mwanzo huku ukiangalia huku na kule, who knows soko la ajira linaweza kubadilika ukapata kazi nzuri tu baadae...shule huwaga ni security kama back up fulani ila sio the ''ultimate answer''
 
Hilo nalo ni neno, maana hawa wazazi wetu bhana alafu nahv unakuwa huna uhakika [emoji1787][emoji1787]
Unajijengea security kwamba ni mzazi wako, kumbe yeye anatumika kwenye ulimwengu tofauti kabisa na wewe........anakufanya asset tu ya kufanikisha mambo yake ya giza na huenda akakutoa kafara kabisa kwa wachawi wenzie. Ndo maana wenzetu majuu ukishafika miaka 18 upo huru kuondoka kabisa kwa wazazi unakuwa independent hata namna unavyofikiri na kuchukulia mambo ikiwemo na mambo ya kiimani bila wazazi kukulazimisha kwa namna yoyote ile.
 
Fanya hata vibarua vya ujenzi ili mle, sasa utafanya nini mama ndo hivyo.

Alitarajia mambo makubwa kwako, hajui subira pia yavuta heri.

Usimkimbie, pambana mwanangu
 
Naona umefungua kamlango ka kutiririsha LAANA....! Vyema ufute uzi na uombe msamaha rohoni wa jinsi unavyomuwazia kumtenda vibaya mama..hutakaa ufanikiwe asilani...! Utabak kushika hela ndogo ndogo tu za kula...! Just an advice!.
Laana ipo...

Imeandikwa;

“Laana isiyo na sababu haimpati mtu”

Na “ enyi wazazi msiwachokoze watoto wenu”

Tafakari.
 
Wahenga walisema "Mtoto Ni Mtoto Kwa Mama Hakui", huwezi kulinganisha hasira na msongo wako wa mawazo ulionao na ile hali aliyokuwa nayo mama yako wakati anakulea ulipokuwa mdogo, tena bila baba yako kuwepo. Unajua alipitia mangapi kukulea wewe akiwa peke yake (Single Mother) bila baba yako? Unajua aliamka mara ngapi usiku wa manane kila mara pale wewe ulipoamka, ulipolia, au kila ulipoumwa, uliposikia njaa au kiu? yeye kukuambia wewe ni mzembe haingii hata chembe ukilinganisha na aliyoyapitia yeye wakati anakulea. Lakini pia kwanini ukereke na kauli kwamba wewe ni mzembe wakati wewe si mzembe!!?? Shida iko wapi au kweli wewe ni mzembe?! Mtu akikuita wewe ni mjinga wakati unajijua kwamba wewe si mjinga, tatizo liko wapi? Ukikereka na kauli kwamba wewe ni mzembe, huenda kuna ukweli kidogo kwamba wewe ni mzembe.

Kwa sasa wewe una hasira na msongo kwasababu mambo yako hayajakaa sawa kama ulivyotarajia, sio kosa la mama ingawa hasira zako wewe sasa unamtolea mama kwasababu ndiye aliye karibu na wewe, hata ungekuwa na mke, rafiki au ndugu aliye jirani na wewe lazima hasira zako ungemtolea huyo mke/ndugu au rafiki, na yeye mama pia ana hasira na msongo na anasikitika kwasababu anaona mwanawe mambo yake hayajakaa sawa na hilo linamsikitisha.

Maneno anayoyasema mama kwako, hiyo ni namna yake ya kuelezea hasira zake, kwa malezi aliyokulia na kwa uzoefu wake hapo yeye anajiona yuko sawa, tambua wewe ni mtoto wake (Hata uwe na miaka mingapi) bado wewe ni mtoto kwake, ana wajibu wa kukusema haijalishi ulimfanyia nini huko yuma - kumbuka mtoto ni mtoto kwa mama hakui. Usithubutu kumsema mama yako vibaya - usithubutu.

Shida iliyopo au shida mliyonayo wewe na mama ni kwamba nyote kila mmoja wenu ana hasira, msongo n,k lakini mmevibeba kichwani mwenu, hakuna anayemwambia mwenzake yanayomsibu au kilichomo akilini mwake na mipango na mikakati yako ya kuondokana na hali hiyo (Badala yake wewe umekuja hapa Jamiiforum badala ya kuongea na mama yako)

Kukimbia, kuuza nyumba au shamba au kumsema au kumwambia kwamba anakusimanga (Haya ni mawazo ya kichwani mwako) sio ufumbuzi. Mnahitaji kuboresha sana mawasiliano kati yenu wewe na mama, kila mmoja bila hasira amweleze mwenzake kinachomsibu kichwani mwake na mipango na mikakati anayopanga ya kuchomoka kimaisha. Hata kama una mipango ya kuondoka lazima kwanza uzungumze na mama kwa utulivu na unatafakari kufanya hivyo na kisha ndio uondoke.

Kama kweli una hasira sana, basi hasira zako kazitolee kwenye kazi, kwenye kilimo, biashara au ujasiriamali na sio kwa mama yako.

Nani kama mama?
 
Kwanza pole sana.

Ushauri wangu,tafuta namna kuondoka hapo nyumbani.

Maana inaumiza sana sasa hasira zinaweza kuja kukupa kufanya maamuzi magumu
 
Pole sana. Usijutie wema uliomfanyia mama yako. Tafuta namna ya kuondoka hapo nyumbani umpishe
 
Back
Top Bottom