Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

'Waheshimu baba na mama yako, upate heri, uishi siku nyingi duniani' Yesu akaongeza, "Amri hii ndio ya kwanza yenye ahadi"

Endelea kuwa na amani na mama yako, msikilize, kuna kitu hujamuelewa, baraka zako zipo kwake, endelea ku fight na kumsaidia, siku moja utashangaa, hii ahadi sio kwa ajili ya watakatifu, ni ahadi ya Mungu kwa watu WOTE

Acha kujipa haki na kajumba kako, kuona Kama vile umemsaidiiiiia!!, ni wajibu wako, mchukulie positive na everything will change soon
 
Huenda mama yako ni mchawi sugu na ndio alishiriki kumuua baba yako sasa anakutafutia sababu ya kukula nyama ukizingatia mahindi umelima mwenyewe
 
Huenda mama yako ni mchawi sugu na ndio alishiriki kumuua baba yako sasa anakutafutia sababu ya kukula nyama ukizingatia mahindi umelima mwenyewe
Wacha kumshawishi kishetani ili amfanyie ubaya mama yake. Kama ni mchawi angemuua tokea hapo awali, leo amekuwa mkubwa ndiyo unamwambia ujinga huo wa ati mama yake mchawi?
 
Ondoka tu hapo home itakua nafuu kwako kuliko kuwaza kuuza mali wala kumzika
 
Pole sana. Kuna wazazi wa aina hiyo. Umesoma, tumia elimu yako ikiwemo pamoja na ku-ignore masimango huku ukiendelea kutafuta.

Tatizo ni umasikini. Wazazi kufikiri kuwa watoto wataondoa kutoka umaskini wao. Na mimi lilipitia huko.
 
Sijui nikwambie nini ila mzazi akizingua jitahidi sana kumulewesha akishindwa kukuelewa bhasi ondoka ukaanze maisha kwingine sio rahisi lakini ni jambo sahihi kufanya.. Mwanadamu yeyote anasahu mapema hiyo ndio asili yetu so mama kwa sasa anakuona mzigo ila Trust me ipo siku atakukumbuka na wewe mfanye akukumbuke kwa wema ONDOKA KWA AMANI.
 
NAOMBA KUJUZWA WANAFUNZI AMBAO WAMESOMESHWA NA BOOM LA UMMA NA AMBAO HAWANA AJIRA, SEREKALI INARUDISHAJE FEDHA ZAKE? "UKIZINGATIA ALMOST 70%HAWAPATI AJIRA"
 
Acha malumbano na Mama...

Wanawake wameumbiwa laana hao, asije akakulaani na usitoboe maisha yako yote,,,, La kufanya achana nae nenda kafanye maisha sehemu nyingine,,,na aga vizuri tu nyumbani...

Amani na mzazi ni muhimu sana kwenye Dunia hii ya sasa...
 
Inawezekana mama amepata lijamaa,anataka wajiachie hapo nyumbani. Sepa zako wala usimtafute kwa muda flani ili ajue umuhimu wako.
 
It pain njoo dsm tupambane hapa kukaa na wazazi kwa umri wako utakufa kwa stress na hizi Familiya za Kia-Africa most of them they know nothing about hard moment yaani they love u Kama hupo na pesa na si kitu kingine .
Hasa Kama Kuna rafiki yako anakuja kwenu kukusalimia yupo njema utajuta utatolrwa mifano wewe mpaka uone hiki nini. ila wamama wa Karne hii ni mtihani wallah
 
Back
Top Bottom