Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Naomba ushauri: Simuelewi mama. Nina hasira sana

Noma ondoka hapo dharau zitazidi kuna mwana alianza kugombana na mama ake ivyo ivyo 😅😅😅😅Kama mke mwenzie kila siku kusemwa na ni wakiune kashatoka mwaka uuishe huu anauza viatu
 
Omdoka,si unajua mama anaumia anavyokuona kijana wake upo tu home bila mchongo wowote,

Usiuze nyumba aisee,bora uuze vitenge vyake upate mtaji.

Hakuna mzazi anefrahia kubanana na mwanae nyumbani bila sababu,
 
Cjui kama utawaza kama mimi ..... pia hujataja mkoa uliyoko kwakifupi ingekuwa ni mimi natokomea kusiko julikana walau kwa miaka 2 au 3 ila kuwa na mawasiloano yake tu ... piga kazi kama vile umetumwa na kijiji MUNGU huwa hamtupi mja wake ... utakuja nishikuru
 
Kama mama yako mzazi anakuambia ayo maneno uza shamba muachie nyumba fanya kuondoka hapo
Wewe ni mwanaume ela uitumie vizuri
Huu ni moja ya ushauri wa HOVYO kabisa kutolewa; Unamshauri auze shamba kwani la kwake?
Lakini pia atakaye nunua Nyumba au shamba kutoka kwa mtoto wa 20s bila kufuatilia kwa mtendaji/uongozi atakuwa hajitambui. Yaani unamtafutia laana kutoka kwa mama yake ya kumfanya asiweze kushika pesa maisha yake yote!!!!
Wewe mshauri aondoke hapo nyumbani akajitafutie cha kwake; acha kuwazia mali ya Urithi
 
Naandika kama muhenga hapa
Kwa ushauri wangu huyo ni mama yako mzazi na binadamu tuna mapungufu yetu na hata kuna mambo ambayo huwa yanatuvuruga ila tunashindwa kuyaweka wazi

Hapo ndio linakuja suala la kufoka hovyo bila sababu au tuhuma za kila aina kama mama yako anavyofanya

Baba yako alifariki ungali bado mdogo sasa leo umekuwa mkubwa Hebu muache mama akae na mwenza hapo wewe unaondolea kwa njia nyingine ila hataki kukuonyesha kama mwanae wa kumzaa

Siyajui maisha ya kila mtu ila mambo haya yapo sana
Hama baba nenda katafute maisha kwingine yeye nenda kamtembelee tu

Kwani umezaliwa peke yako? Kama ni hivyo pole pia ila mama ni mama mpe Uhuru wake pia hata kama anataka kuwa peke yake sawa tu
Ila hataki kukuambia ukweli she loves you
 
Nillelewa na mama baada ya baba kufariki nikiwa mtoto mchanga. Kwa hali hiyo Nilisomeshwa na wasamaria wema.

Nilipokuwa nasoma college nilikuwa nanjibana sana namtumia mama yangu 35% ya kila mkopo wa kujikimu, yaani boom. Nilifanya kazi za zege ili pesa nitakayolipwa nichanganye na kiasi cha boom nimjengee mama kijumba cha bati na choo. nilifanikiwa kwa hilo hadi umeme nimevuta. Wenzangu walijibana wakanunua pikipiki ambazo sasaivi wanazifanyia hiashara ila mimi nilichangua kujenga nyumbani. Nilipanga ghetto la hali ya chini kuliko wanafunzi wote pale chuoni. Sikubadili nguo kama wenzangu. Nilivaa nguo moja hadi ikapauka, nilipiga nyeto kukwepa kuhudumia dem, kwa kifupi niliishi maisha very identical ili tu kubana boom kwaajili ya kumuwekea mama mazingira yanayoeleweka.

Nililipomaliza college kumekuwa na changamoto ya ajira hivyo nipo nyumbani muda mrefu. Mama amethubutu kunigombeza kwamba mimi ni mzembe na huwenda nilikuwa malaya chuoni ndiyo maana sikuweka akiba ya boom ambalo lingenisaidia kuanzisha biashara kama wenzangu! Yaani amesahau?! Naona amefikia hatua ya kunisimangia chakula, tena ambacho nimelima kwa nguvu zangu.

Hasira ziliniwaka na hapa nataka nimdanganyie safari ya kwenda kuwatembelea ndugu zake Iringa ili nibaki mwenyewe niuze nyumba na shamba na kutokomea town. Wakati mwingine waza kumzika


Take it as an inspiration and not a hate..Itakusaidia siku usiuze chochote baraka zako ziko chini ya miguu ya Mama...be humble and God will make a way for you bro..
 
Huyo ni Mama yako,mueleweshe tu ila hata asipokuelewa wewe mvumilie tu na uondoke hapo home ukapambane ila usimsahau Mama yako wala usimfanye kua ni adui yako,

Kumbuka huyo Mama yeye alikuvumilia mambo mangapi toka ukiwa mchanga mpaka leo hii umekua mtu mzima,

Alivumila mengi sana na kama usemavyo Baba yako alifariki toka wewe ukiwa bado mtoto mchanga,

Achana na fikra za kumkomoa Mama yako,tumia hizo lawama zake kwako kua hasira ya kutafuta hela na sio kumjengea chuki,

Good luck Bro.
 
Back
Top Bottom