Naomba ushauri wa biashara ya malori

Ndio imesha wezekana!
Beyond economic repair...
Gari zote zinaharibika beyond economic repair huoni ambavyo haukuwa serious na mali zako?

Wenzako wametengeneza kuaminika kwa wauza vipuli, anakopeshwa anarekebisha tatizo!
gari ikirudi deni linalipwa maisha yanaendelea..

Kama huna mapenzi na magari, hizo harakati zote utaona ni usumbufu mkubwa na lazima uyatelekeze tu!!

Nisikulaumu mkuu, na imani unafanya vizuri kwenye nyanja nyinginezo..
 
Nimeamua kwenye trailer hapo nianze na ya kukodi nione kwanza pesa inavyoingia. Ahsante Mkuu
Mktaba wenu
1. Niliona umetaman trailer ya super single, je airbag ikipasuka gari inaingia mizan nani analipa?
2. Tyres iki burst nan analipa, kawaida kwa super single
3. Service ya trailer , imekatika sehemu inahitaji kuchomw nan analipa?


Ukiona hayo maswali majibu yana ukakasi

Unga unga trailer upate yako.
 
Mimi nimempa ushauri kutokana na uzoefu wangu!
Nashangaa unamshambulia mshenga!
Na ww mpe ushauri wako! mf; pale brake shoes zimeisha unaenda nunua mpya na kufunga ukiamini ni mpya!; baada ya dereva kuendesha gari 12.km anashika brake haishiki!; kuja kucheck brake shoes zote zimeungua zilikuwa fake!
Mungu Amenusuru hakukuwa na Ajali!
Nakuomba mpe ushauri hapo!
Mimi nimesha inua mikono kugombana na mavyuma!
 
Ahsante sana kwa kunifungua macho pia, nilikuwa nikiwaza hivyo kabla ila baada ya kupokea ushauri wa wengi nadhani double tyre itakuwa nzuri kwangu. Naendelea kupokea mapendekezo na kuyadadavua zaidi. ahsante sana kwa ushauri mwamba!!
 
S unarud ulipo nunulia unamkamata unapeleka mahakaman
 
Kama tungeendelea na huu mjadala, ungegundua udhaifu ulipo..

But samahani pia kama umekwazika mkuu!
Didn't intend to do so!

All the best..
 
Ingekuwa rahisi kihivyo kumshika simba ndevu!
Mkuu ww uko bongo??
Unaujua shina la mtandao wao[emoji24][emoji24][emoji24]
Pole sana mkuu

Tajiri wa kwanza wa hovyo kuwah kukutana nae..itakua mali ya urithi
 
Nimedadisi sana kuhusu hili, super single kwa maana ya trailer nimeambiwa inabeba mzigo mwingi kwa sababu trailer inakuwa nyepesi kulinganisha na trailer yenye double tires
Hapana mkuu, super single haibebi mzigo zaidi ya double Tyre. Nimekuwekea hapa sheria ya mizigo ya east Africa ambayo ndo sheria mama hapa Tanzania linapoluja suala la weight.
Kuhusu budget na aina ya gari unayotaka kununua Upo sahihi na karibu kwa game.
 

Attachments

Samahani Mkuu, cummis ni nini?

Halafu hiyo R500 unayomshauri jamaa hazifiki hata tano nchi nzima!

Superstar & world oil ni miongoni mwa wenye mbavu za kununua hii gari lakini hawana..

Muache jamaa atulize roho yake kwenye 124!!
Cummins ni engine za kimarekani kwa sasa nyingi zipo kwenye mabus ya kichina na gari za muitaliano kama Iveco
 
Hizi Trailer za kukodi zipo wapi? Natafuta semi trailer ya box body
 
Pole sana mkuu

Tajiri wa kwanza wa hovyo kuwah kukutana nae..itakua mali ya urithi
Hizo ni ramli unazo piga!
Mimi nimeweka ukweli wa changamoto nilizo pitia!
Ndio sababu hata mleya uzi nilimshauri kama Atazimudu hizo changamoto atashinda!
Ooh Mali ya urithi sijui mzuwanda huyo...
Ninaamini msemo wa wahenga kwamba mhadithia mvua imemnyea.
 
Unakubalije mtu akutie hasara? Alafu unamwacha tu, huna uchungu na mali yako au pengine ulisha ridhika

Kwa tafsiri yeyote yule mtu yeyote atakae fanya upuuzi huo kwenye mishe zangu apotee tu mazima, nitakula nae sahan moja

Mtu anakurudisha nyuma unamwangalia tu? Hata gari zako inawezekana kabisa watu walikusaidia kuziua kwa kukuuzia vipuli fake
 
Nimetulia nachezea Ardhi Ambayo Haimtupi Mtu!
Kuliko kupambana na upepo kwenye maisha haya mafupi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…