Naomba ushauri wa biashara ya malori

Naomba ushauri wa biashara ya malori

Nimedadisi sana kuhusu hili, super single kwa maana ya trailer nimeambiwa inabeba mzigo mwingi kwa sababu trailer inakuwa nyepesi kulinganisha na trailer yenye double tires
Kwa horse ya 6x2 trailet ya supper single ipo rated na Tanroad kubeba gross 48500kg , ya double ipo rated 50000 kg ni rahisi sana ku overload trela ya super single kuliko ya double bed
 
Cummins ni ya wamarekani mzee, kwenye scania 4 series inatafuta nini asee?
Cummins ni engine ya kimarekani ,wakati europeans wanaingia tier 3, emissions control , manufacturers pekee aliyekuwa na nozzle simple ku meet euro 3 standard alikuwa ni Peugeot(France) na tech yake ya unit injector , 'pump duce ellementer' (PDE)
Truck manufacturers waliopoona wangekuwa nje ya standards wakaamua kwenda kununua tech hii kwa mfaransa , kwa masharti kwamba neno PDE liwe ni lazima kuwa included kwenye kila engine itakayo tumia tech hiyo kama copyright za france tech
Miongoni wa watengenezaji walolipa kutumia tech ya PDE alikuwa ni cummins , volvo , scania etc na nozzle hii wote walienda kutengeneza kwa Bosch germany. Bosch alichofanya alitengeneza nozzle hii kwa stlye na dimensions moja akaja kutofautisha juu tu kutokana na cam na valve configuration kwa gari husika .

Cummins ilikuwa ya kwanza kuja Tanzania nyingi zilikuja kama gensets , mafundi wakakariri nozzle , ilipokuja 124 420 na unit injector mafundi wakaibatiza scania Cummins.
 
Hizi Trailer za kukodi zipo wapi? Natafuta semi trailer ya box body
Kwenye trucking, trailer ndo gari yenyewe, trela zinazokodishwa huwa ni trela dhaifu na mara nyingi zinakuwa very expensive to maintain.
Kupata trailer iliyosimama ati inakodishwa sio rahisi labda kama gari ilikuwa ni moja na labda imekufa au kupata ajali
 
Mende ya mchanga haiwezi kukaa meza moja na semi kwenye kurudisha pesa .
1. ni gari ya gharama kuanzia manunuzi hadi service kwa sasa mende used ipo kwenye 120 plus , manunuzi tu
2. Ni gari ya msimu, kukinyesha mvua gari ya mchanga inapaki uani just like fuso tipper
3 njia inazopita mende za mchanga si rafiki kwa gari na vitu kama kuvunja diff springs, gearbox , crossmembers , center rubbers , chassis , boggies ni kawaida kwa tipper ya mchanga
Mende ni nzuri kama una project zako binafsi za ujenzi
Gari za EU au Scandinavia huwa ziko well spec'd na zinakuwa hazijatembea sana, tatizo ni LHD.
 
Attachments

  • tractor-unit-SCANIA-R620-LB-8X5-HSZ-Euro-5-Hydraulik-Nybesiktigad---1653290762831798741_big--2...jpg
    tractor-unit-SCANIA-R620-LB-8X5-HSZ-Euro-5-Hydraulik-Nybesiktigad---1653290762831798741_big--2...jpg
    57.2 KB · Views: 83
Well speced ni kweli , ila kutembea hapana hao jamaa magari yao mengi yana km nyingi , ila kqa kuwa yanakuwa well speced gari hizo hata ukute ina km milion 2 , bado inakuwa smart.
Vipi kuhusu kuwa LHD, haiwezi kuwa accident prone kwa mazingira yetu ya kibongo.
 
Kwenye trucking, trailer ndo gari yenyewe, trela zinazokodishwa huwa ni trela dhaifu na mara nyingi zinakuwa very expensive to maintain.
Kupata trailer iliyosimama ati inakodishwa sio rahisi labda kama gari ilikuwa ni moja na labda imekufa au kupata ajali
Hizi trailer za mTuruki vipi ubora ukilinganisha na German trailers used.
 
Nimesoma comment zote,ila cjaelewa super single na double tires ,nawasilisha jf
 
Hizi trailer za mTuruki vipi ubora ukilinganisha na German trailers used.
Trailer sio kama horse , tariler ubora unapimwa kwa componets au part zilizotumika kuunda tela hilo,

Kwanza kabisa ni axles, hizi zipo aina nyingi kam vile Ror, Saf, piacenza, bpw, fuwa etc , to the best of my knowledge bpw ni axle nzuri kuliko zote ,
Pili ni braking system , hapa kuna wabco , knorr bremse , bendix etc , nzuri again naona ni wabco
Mturuki na mjerumani wana options zote , ubora wa trela utategemea aina ya components zilizotumika .
 
Nimesoma comment zote,ila cjaelewa super single na double tires ,nawasilisha jf
Double tires ni mfumo wa matairi mawili yanayofungwa pamoja kwenye axle , nina uhakika umewahi ona kwenye basi au lori yale matairi ya nyuma au ya kwenye diff ni double !
Super single sasa ni tairi moja lenye uwezo wa kufanya kazi peke yake , badala yale mawili kwa pamoja , neno super linatumika kuonyesha uimara wa tairi hilo
Huko america hata drive tryes huwa wanatumia super single, huku africa na ulaya super single inatumika kwenye trailer ,mbele au lifting tag axles.
 
Kiongozi kongole kwa uelewa n shule unayotoa hapa
 
Double tires ni mfumo wa matairi mawili yanayofungwa pamoja kwenye axle , nina uhakika umewahi ona kwenye basi au lori yale matairi ya nyuma au ya kwenye diff ni double !
Super single sasa ni tairi moja lenye uwezo wa kufanya kazi peke yake , badala yale mawili kwa pamoja , neno super linatumika kuonyesha uimara wa tairi hilo
Huko america hata drive tryes huwa wanatumia super single, huku africa na ulaya super single inatumika kwenye trailer ,mbele au lifting tag axles.
Jf ingekuwa inatoa like Kwa rating mm ninge toa zote ,umetoa shule nzuri sana muheshimiwa
 
"Kila unachokiona mbele yako kilishawahi kuwa kwenye truck"

Umeamua vyema kuwaza biashara hii.

Niongeze kidogo

Kuliko kununua gari used budget yako inatosha kuwapa TATA wakakupa gari mpya kwa 35m na trailer ukiunga unga utapata kwa 30m double tyres.

Super single ina changamoto nyingi sana kuliko unavyoweza kudhan!
Transcargo, Dangote hawana trailer za super single.

Ukiamua kuchukua gari used jitahidi kuipitia kila sehemu ikiingia barabaran usipate changamoto. Maghari yanayotoka Poland usichukue mengi yametumika sana.

Gari kutoka South Africa ukipata muungwana akakurekebishia kabla ya kulisafirisha ni gari bora kuliko mtumba wa Uingereza.

Ukiamua kuchukua Uingereza hakikisha MOT iko active hii gar imejaribiwa kwao na inafanya kazi katika barabara za Uk.
Scani 124 420, kuwa makina kuanzia 2002 hadi 2004 nying ni HPI ama red dot zinasumbua sana katika mazingira yetu.
6x2 chagua tag axle yaan teriaz nyuma ili uweze kubeba mzigo mkubwa.

Biashara ni nzuri ngumu, jitahidi ujibanze kwenye kampuni yenye kazi za uhakika. Kazi za dalali zitakufanya uchukie kazi.

Usimamizi jitahid mda mwigini uone gari nanufanye service.

Hayo machache kwa nilivyojionea barabaran.
Mkuu ushauri wako nimeufanyia kazi sana, Kuna gari nilichagua nikaomba nipate MOT nifanyie tracking online. Supplier akabaki kuniambia its still valid up to next year sijui mwezi gani huko. kila nikiomba anitumie namba niicheki hatumi. Nikaogopa nikakumbuka huu ushauri. Hivi hizi MOT huwa wanatuma kweli ili na sisi tujiridhishe. Tupe experience yako Mkuu.
 
Mkuu tunaweza kuwasiliana??? Nina experience na kazi hii zaidi miaka 10

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Kwenye trucking, trailer ndo gari yenyewe, trela zinazokodishwa huwa ni trela dhaifu na mara nyingi zinakuwa very expensive to maintain.
Kupata trailer iliyosimama ati inakodishwa sio rahisi labda kama gari ilikuwa ni moja na labda imekufa au kupata ajali
Mmh jamani ongea lugha moja b
hac
 
Back
Top Bottom