Naomba ushauri, wazazi wangu hawataki nisome ujuzi mwingine zaidi ya taaluma niliyosoma

Unachoweza kufanya sasa fanya usingoje maana aisee miaka inaenda kasi.
Mimi kuna muda natamani ningerudisha umri nyumba nikiona vijana wanacheza na muda walionao.
Asante. Kweli ni changamoto kusubiri kila kitu kitokee bila kujishughulisha au kupenda mteremko
 
Ni mtoto wa 5 kati ya 7 tuliozaliwa.
Nimesomea sheria.
Ni kawaida watoto wa katikati kudharauliwa,wakati mwingine kutopata ushirikiano wakaribu.Kama umeshahitimu digrii yako, we tayari ni mtu mzima; hatima ya maisha yako, yako mikononi mwako. Fanya kile kitu akili yako inataka kwa sasa ili kutimiza lengo lako. Wazazi wape heshima yao, ila hawatakiwi kukupangia maisha
 
Asante kwa mawazo yako mkuu.
 
Mtoto mjinga sana wewe...kaa nyumbani kula chakula ushibe na upumzike..unataka kwenda wapi ?..umefukuzwa....usituletee tabia za upigaji za tamisemi hapa
 
Sijawahi kuwasusia wazazi wangu. Sema tu ni ile type ya wazazi ambao ni wakali sana haswa mama yangu! Kiasi kwamba inakua ngum kuwa karibu .. na kuna hali flani ivi ya kutojiamini maana kila unachofanya unakosolewa bila kuambiwa nini cha kufanya!

Basi jaribu kuongea na baba yako bila kuwa na mama, na ikwezekana mwambie namna unavyojisikia kutokana na treatment yao kwako.
 
Asante ndugu yangu.

Nilishafanya utafiti wangu kwa eneo nililopo nimepata chuo kimoja ambacho ni affordable na wanafundisha magari aina yote yani manual na automatic.
Good ukijua manual utakuwa umejua kuendesha Gari zote nakushauri komaa na manual maana automatic hufundishwi unaelekezwa
 
We ni wakishua kama waliweza kukupa 3000 kila siku itakua wanayo plan kwaajili yako, tulia hapo uendelee kuwaskiliza nisije nikakupa ushauri mgumu kuliko uwezo wako yakakukuta magumu zaid alaf urudishe tena mpira kwa kipa
 
Hatma ya maisha yako Iko mikononi kwako. Wazazi tunawapenda na kuwaheshimi lakini sometimes maamuzi ya maisha Ni yako.

Mimi nlisoma chuo nje nlipomaliza mama Yangu alikuwa anipigia kelele rudirudi huko unafanya Nini wakati ushamaliza. Si nikasema ngoja nimsikilize, nikarejea bongo.

Nlichokutana nacho najuta sijawahi kumwambia najuta lakini nlijifunza maamuzi yangu binafsi mzazi Nampa tu Taarifa, akubali akatae me nitafanya maamuzi.
 
We ni wakishua kama waliweza kukupa 3000 kila siku itakua wanayo plan kwaajili yako, tulia hapo uendelee kuwaskiliza nisije nikakupa ushauri mgumu kuliko uwezo wako yakakukuta magumu zaid alaf urudishe tena mpira kwa kipa
Ingekuepo plan wasingesita kunishirikisha, na mtu mwenye plans huwa dalili zinaonekana
 
Pole pia .. kuna vingi vya kujifunza
 
Nadhan ukimya wako haukuwa suluhisho,ungejenga utaratibu wa kuzungumza na wazazi wako kuhusu changamoto unazopitia,kama wamelipa ada basi wanakujali sana.Pia inaonekana wazazi wako ni protective sana pia ni wakoloni,sioni kama wana nia mbaya na wewe ni hilo tu.Nachokushauri tafuta namna nzuri ya kujenga hoja zako na kuziuza kwao,tumia namna yenye ushawishi mzuri,wafanye waone umuhimu wa unachotaka kufanya...wataelewa,kama hawaelewi,sababu ni ndoto zako na unataka kuzisimamia WAFANYE WAELEWE na simamia unachoamini...Mwisho kabisa kuwa makini na wanaume wa humu.
 
Weka kapicha tuone inawezekana wazazi wako sahihi
 
Asante sana. Nmekuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…