Naomba ushauri, wazazi wangu hawataki nisome ujuzi mwingine zaidi ya taaluma niliyosoma

1. Nipate skills, chochote kinaweza kutokea, nina plan ya kufanya biashara ambapo ni vyema kujifunza gari

2. Upishi nitasoma tena baada ya kuwa dereva.

3. Nmesomea sheria.

Nashukuru kwa kujibu maswali yote.

Sasa tuanze.

1. Kwanini usijiendeleze kwenye sheria? Kwa pesa uliyo nayo kwann usiende Law school? Nasema hivi kwa sababu mtu aliueenda law school ni rahisi kupata p kujishikiza tofauti na mtu ambe hajaenda! Na kama ukiwa na akili basi hutalala njaa kama una muhuri!

Unless kama hupendi sheria basi unaweza fanya tofauti na huo ushauri!

2. Unasema unataka ujifunze gari ili ulitumie kwenye mishe zako je una hela ya kununua gari kwa sasa? Kama huna kwann hiyo ela ya ada ya udereva usifanyie kitu kingine?

3. Kwasababu umesema unapenda upishi kwann usifikirie kujiajiri kwenye upishi kuliko hiyo kulipia ada ya udereva wakati hata gari huna (wenda hata wazazi hawana)?

Ushauri... mwingine!

Kama una laptop pia unaweza fanya haya na yakakusaidia bila kutumia hiyo ela yako kwenye ada ya udereva..

1. Jifunze social media marketing ukafanya kazi za freelancing. Uzuri huu ujuzi utakusaidia hata kwenye biashara zako za ndani!

2. Jifunze copywritting... hii nayo unaweza fanya kazi watu wa ndan na nje (freelancing)! Uzuri ni kwamba umesoma law hivyo na assume lugha inapanda!

Yangu ni hayo kwa sasa! Ila wazo la udereva kwa sasa naona ni illogical decision!
 
Kwanza hiyo pesa uliokuwa una bana matumizi unatakiwa utubu kwa wazazi maana ni kosa kwa Mungu
Pili hayo maamuzi unayotaka kufanya wewe mwenyewe huwe makina wakati unayatekeleza . Waswahili wanasema “mwenye kulitafuta utalipata “ inawezekana ikawa positive au Negative inategemea njia utakazopita.
 

Wazazi watakulemaza, wewe chapa laba, ingia kitaa ukaanze kulipa Kodi na Tozo
 
Pole
 
Ndo wazazi mjifunze kuwa karibu na watoto wenu. Usipomjengea mazingira mtoto ya kuzungumza nae inapotakiwa ndio matokeo yake haya. Inaumiza sana watoto basi tu!!

Na wazazi wetu wa kitanzania wanaona huo ukali na mtoto kukuogopa ndio kuwa mzazi bora[emoji2297]
 
Kama una mtaji wa kutosha!!!!! hapo nyumbani, unasubiri nini? changanya miguu, nenda mkoa wa mbali huko, kapambane na maisha. Ukiendelea kukaa hapo utalemaa afu utakuwa under rule, huwezi kuwa mtu mzima, wee utaendelea kuwa mtoto tu.

Na huko uendapo ukikubali kudanganywa na mwanaume/wanaume, ukaona unapendwa ukakubali shauri zako.

Au ukienda kujiingiza kwenye makundi ya ajabu shauri zako. Ukajisimamie mwenyewe na uwe na msimamo.
 
1. Sina plan ya kwenda law school kwa sasa.. bila kujua ramani kamili ya maisha yangu. Nitaenda baadae, naweza kufanya vitu tofauti na taaluma niliosomea.

2. Sina pesa ya kununua gari, ila kaka yangu anayo hana kazi nayo kwa sababu muda mwingi anautumia kazini, nimeshaongea nae.

3. Upishi ni plan yangu baada ya skill ya udereva ninayoweza kufanya kisomi zaidi.


Asante kwa ushauri wako ila hivyo ni vipaumbele vyangu kwanza kabla sijaingia kwenye fani nyinginezo.
 
Sijakuelewa unachomaanisha
 
Ni tatizo la saikolojia kwa malezi yetu kuwa hivyo.
 
Asante, ila si vyema kumfikiria mtu negative.. sina michanganyo unayoizungumzia. Ni kati ya vitu vinavyokatisha tamaa na kumkosesha mtu amani!

Hapa wazazi wengine ndipo wanapokosea pia!
 
MY SISTER WHATEVER THE CASE NI MUDA WAKO WA KUTIMIZA NDOTO ZAKO... Uzuri ushakua mtu mzima unajitambua, nikutakie kila lakheri Mungu awe nawe...
USIOGOPE
 

Kwa sababu ulikuja kwa kuomba ushauri basi nikakupa ushauri. Ila kwa hali uliyopo bado sijaona logic ya kutumia pesa yako kwenye ada ya udereva kwa sasa!

Anyway muda ni ukuta, fanya maamuzi mema.

Kila la heri.
 
Kwa sababu ulikuja kwa kuomba ushauri basi nikakupa ushauri. Ila kwa hali uliyopo bado sijaona logic ya kutumia pesa yako kwenye ada ya udereva kwa sasa!

Anyway muda ni ukuta, fanya maamuzi mema.

Kila la heri.
Nashkuru kwa ushauri wako ndugu.
 
I'd suggest usisomee kwanza driving, au kama huna shida ya cheti nicheki nitakufundisha...sema utaweka mafuta tu.
Na kuhusu leseni utapata kwa 95k

Mawazo yangu ilikua hio hela ambayo ungeitumia kwa driving ndo ungeenda kujifunza mambo ya upishi ili uweze kua well na skills nyingi za upishi.

Maana umesema kuna shughuli utakuja kuzifanya za kutumia gari, its well known kwa sasa huwezi kununua gari, ko labda utaishia tu kukodisha ambayo inakua cost nyingine zaidi plus ile hela ambayo uliendea driving inakua imeenda bure maana gari umekodisha.

Maybe kama una uwezo wa kupata gari baada ya kua umejifunza then you can go for driving.
 
Nashkuru mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…