Naombeni msaada wa mawazo mwanangu hapendi Kula

Wangu bila Baby Shark chakula hakishuki, wakati wa kula ni kuimba na kupiga ngoma, watoto!πŸ™ŒπŸ»

Fata ushauri wa Jewel_ utasolve tatizo ni kawaida kwa watoto kutokupenda kula hasa akiwa mtoto peke yake ndani hana wa umri wake
Nashukuru sn
 
Mpe therapy ya vitamin ile yenye mchanganyiko wa strawberry atapata hamu ya kula.

Kingine kama unakaa uswalihini mchanganye na watoto wa kiswahili ambao chakula kwao ni kipengele washindane kula.
Hii kumchanganya watoto wengine imekaa mkao ila mazingira hayaruhusu sio uswahilini. Ntaanza na hyo therapy ya vitamin
 
Mpe dawa ya minyoo + vitamin b afu muache njaa ikimtafuna vizuri atakula mwenyewe,usimshikie fimbo kuwa friendly zingatia wakati wakumpa chakula usimpe peke yake tenga mle wote apate compan.....badili aina ya vyakula na pendeleni vyakula visivyo na viungo vingi wengi vinawakinai
 
Haya usiku huu ni makande yamepikwa na ni matamu kweli mana ni ya nazi ila hapa alipo ameshalia wala sijamchapq na natumia busara sn kumbembeleza ila duuh. Mara aseme shingo ina muuma mara aseme kidonda kinawasha. Anamchubuko kwenye goti.
Nacheka tu na hasira zinapanda pia natamani niwawekee kavidio kasekunde kazaa nimrekodi😁
 
Sawasawa shukrani
 
Mnunulie hii kitu utanishukuru baadaye wanauza 25k
 
Umejaribu Chips kuku kidali akakataa?
Nina mtoto anaelekea miaka 3,na yeye ana tatzo hilo hapendi kula na wakat wa kunyonya,kanyonya haswa na alikuwa anapenda sana na mama yake alijitahid sana kumnyonyesha kwa miaka yote miwili

Yaan hata hana mwili,chakula ambacho kidogo anajaribu kula ni wali wenye mchuzi wa maharage na vitumbua

Lakin vitu vingine hapend,nyama na samaki anatafuna baadae anatema,watoto wengine wanapenda sana maandaz lakin yeye hana habari nayo,tukinunuaga chips hizo ndo hana hata habari nazo kabisa anaishia kunywa soda tu
 
Duuh kuna watu wametoa madini humu kwenye huu uzi tujaribu kufuata huenda tukafanikiwa. Chakula ni vyema ale kumuepusha na magonjwa
 
Hivi watanzania mna nini na ukatili? Kila mtu ni katili na hudhani viboko ndiyo njia ya kutatua matatizo ya watoto!
 
Nna uhakika asilimia 80 ukienda mpima damu utaambiwa iko chini..em jaribu kwa wiki moja tu kumpa vyakula vya kuongeza damu utaona mabadiliko, naongea kutokana na experience ya wanangu mwenyewe.
Sawa sawa ntafanya ivo
 
Hakikisha unapika chakula anachokipenda. Mimi kwangu watoto ndo wanapanga menu. Muulize unataka kula nini.. Then pika chakula anachokitaka.

Asipokula au akila kidogo usimlazimishe muache hadi njaa imkung'ute kisawa sawa ataomba mwenyewe chakula.

Unajua hii mambo ya kula asububi mchana na jioni ni mazoea tu. Ila mtu anatakiwa ale pale anaposikia njaa.

Swala lingine, Je mtoto yuko active? Anacheza michezo ya kutumia nguvu.

Hakikisha mtoto anacheza michezo ya kutumia nguvu, lazima atasikia njaa tu. Lakini kama anakaa ndani siku nzima ni changamoto.

Summary

Usimlazimishe, akisikia njaa ataomba chakula mwenyewe
 
Yaan huwa nakawazia siku kakikutana na ugonjwa mkubwa si tunaweza kukapoteza kabisa

Bahat nzur mama ake yupo makin,anajitahid kukatibu haraka kabla mambo hayajawa makubwa
Duuh jitahidi mtaalam. Tukifikiria hayo moyo unapata ganzi
 
Mcheki Dr Janabi, atakueleza kati yako wewe na mtoto wako nani mwenye tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…