Naombeni msaada wenu kimawazo, pesa ama kazi ndugu zangu

Mkuu kwanini usiende kujishikiza security companies kama GARDAWORLD, INSITE, G4S na nyinginezo mshahara kwa mwezi 370,000 hadi 430,000 kwa normal guard
Nani kakwambia Mshahara wao ni huo? Umewahi kujaribu kufanya hizo kazi?
Unazijua CHANGAMOTO zake?

Mleta mada pambana kitaa utatoka usiingie kwenye hayo Magereza sio km unavyoaminishwa unachoambiwa SIVYO kilivyo
 
Wewe jamaa ni muongo sana, usiwapoteze watu maboya watu wapo serious na maisha ikiwezekana hata kuzamia Canada US France na kwingine Ila simshauri mtu awe Mbwa kamwe
 
Simshauri mtu aingie huko, vijana komaeni na mtaa mtaani kuna neema nyingi sana kuliko mnavyofikiria
 
Kwa ulichosomea umejaribu ku apply kwenye auditing fames au hata kwenye hawa clearing agents ila kwa namna ulivyoielezea shule yako kuna ki2 hakiko sawa like hy tra tax officer ndo kitu gani?anyway Mungu akutangulie kwenye hitaji lako
 
Usije ukathubutu ukapeleka ndugu yako huko,
Hapanq ..nilikua nauliza tu mkuu, maana japo mi ni mjasiriamali wa kawaida tu ila nalipa vijana wangu zaid ya hiyo pesa plus breakfast n lunch. Sasa kwann kaz ngum kama hiyo na ya hatar malipo yanakua duni namna hiyo?
 
Ni zaidi nyoko sana ni kuna ukandamizaji huko Dunia nzima hakuna, alafu wanawachukulia Mbwa wote walionona ni maboya hawana akili km una ndugu yako kamwe usije ukamshauri aingie huko
Ni nomaa
 
Una passport
 
Hapanq ..nilikua nauliza tu mkuu, maana japo mi ni mjasiriamali wa kawaida tu ila nalipa vijana wangu zaid ya hiyo pesa plus breakfast n lunch. Sasa kwann kaz ngum kama hiyo na ya hatar malipo yanakua duni namna hiyo?
Hakuna meal allowance
Hakuna health insurance
Hakuna promotions
Hakuna salary increments
Hakuna haki za mfanyakazi

Hivyo ni baadhi tu list ni ndefu
 
Nimefatilia michango mbalimbali ya wadau, lakini ngoja nikwambie kitu mtoa mada. Kwenye Aya maisha kabala ujafanya maamuzi angalia kwanza wewe mwenyewe unataka kufanya Nini. Kuna mchangiaji hapo juu ameongea Jambo zuri sana, ukiwa katika utafutaji usipende kutanguliza elimu katika Dunia hii, hivi unajua ni watu wangapi walioko mtaani na elimu kama Yako lakini hawana kazi?.

Fata ushauri wa mdau hapo juu, Nenda kwenye kama Gad world, SGA, G4S, usiende kwenye kampuni tofauti na hizo nilizokutajia, Peleka maombi endapo utachaguliwa kujiunga. Ukiwa katika hatua za mwisho kupangiwa sites mwambie kiongozi akupeleke Zanzibar Kuna siku utanishukuru, ukisikia kiongozi anasema wanaotaka kwenda zanzbar mwambie akuweke kwenye list.Ukipata nafasi ya kwenda Zanzbar ni poa sana maana kule site nyingi ni mahotel makubwa ya kitalii, kwaiyo unakaa Camp Bure, unakula Hotel NK. Pesa Yako unatunza, ukipambana mwaka mzima umepata mtaji. Wanao kwambia siju mshahara ni 120000. ni ungo kabisa, Zanzbar milinzi wa G4S, Gad world SGA analipwa Hadi laki 4 ukubali ukatae Mimi nilipita uko.

Kingine ni kwanini ukomalie Dsm tu?, Ni kwanini vijana wengi mkmaliza vyuo hamtaki kutoka kwenye Hilo jiji? Kama vipi badili mazingira njoo hata mikoani ucheki furusa nyingine, Fact ni kwamba jiji la Dar limeshabana Yani kutoboa ni kipengele kikubwa. Walio nacho wataendelea kuwa nacho na asie nacho anabaki patupu. Badili mtazamo Rudi Hata mkoa upambane. Kwani dar pekee ndo Kuna maisha tu? Yangu ni hayo ukiambiwa kitu changanywa na zako. Maisha hayana huruma, sio Kila mtu anakushauri hapa ana huruma na Wewe, mwambie basi hata uende kwakwe ukale ugali kama atakubari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…