Mkuu acha dharau, nina ndugu yangu alifanya kazi unayoiita Mbwa kwenye moja ya kampuni tajwa, kituo chake cha kazi kilikua GGM.
Aliacha kua "Mbwa" kwasababu kampuni ilipoteza tenda kwenye hicho kituo enzi za Jiwe.
Lakini hadi anaacha kazi mshahara wake ulikua 900k na alikua anakula chakula anachokitaka, analala sehemu nzuri, anafuliwa nguo, yani kiufupi anapata huduma zote bure akiwa kazini.
Na kazi ilikua wiki mbili kazini wiki mbili nyumbani. Amejenga mjengo wake wa maana, kazi ilivyoisha akachuku mafao yake akafungua biashara na ana maisha mazuri tu. Kwahiyo ndugu acha dharau pia jifunze kuheshimu kazi za watu.