Nimefatilia michango mbalimbali ya wadau, lakini ngoja nikwambie kitu mtoa mada. Kwenye Aya maisha kabala ujafanya maamuzi angalia kwanza wewe mwenyewe unataka kufanya Nini. Kuna mchangiaji hapo juu ameongea Jambo zuri sana, ukiwa katika utafutaji usipende kutanguliza elimu katika Dunia hii, hivi unajua ni watu wangapi walioko mtaani na elimu kama Yako lakini hawana kazi?.
Fata ushauri wa mdau hapo juu, Nenda kwenye kama Gad world, SGA, G4S, usiende kwenye kampuni tofauti na hizo nilizokutajia, Peleka maombi endapo utachaguliwa kujiunga. Ukiwa katika hatua za mwisho kupangiwa sites mwambie kiongozi akupeleke Zanzibar Kuna siku utanishukuru, ukisikia kiongozi anasema wanaotaka kwenda zanzbar mwambie akuweke kwenye list.Ukipata nafasi ya kwenda Zanzbar ni poa sana maana kule site nyingi ni mahotel makubwa ya kitalii, kwaiyo unakaa Camp Bure, unakula Hotel NK. Pesa Yako unatunza, ukipambana mwaka mzima umepata mtaji. Wanao kwambia siju mshahara ni 120000. ni ungo kabisa, Zanzbar milinzi wa G4S, Gad world SGA analipwa Hadi laki 4 ukubali ukatae Mimi nilipita uko.
Kingine ni kwanini ukomalie Dsm tu?, Ni kwanini vijana wengi mkmaliza vyuo hamtaki kutoka kwenye Hilo jiji? Kama vipi badili mazingira njoo hata mikoani ucheki furusa nyingine, Fact ni kwamba jiji la Dar limeshabana Yani kutoboa ni kipengele kikubwa. Walio nacho wataendelea kuwa nacho na asie nacho anabaki patupu. Badili mtazamo Rudi Hata mkoa upambane. Kwani dar pekee ndo Kuna maisha tu? Yangu ni hayo ukiambiwa kitu changanywa na zako. Maisha hayana huruma, sio Kila mtu anakushauri hapa ana huruma na Wewe, mwambie basi hata uende kwakwe ukale ugali kama atakubari.