Naombeni ushauri juu ya mtoto asiyepelekwa shule kisa hakuna ada

Hili swala linatakiwa lianzie ngazi ya familia, wazazi wenu wapo, ndugu zenu wapo, fikisha shauri lako kwa pande zote mtatue hii changamoto

Level ya wazazi ikishindwa kufikia muafaka peleka shauri lako serikalini ustawi wa jamii. Ufumbuzi utapatokana na kama wataona wewe unafaa kukaa na mtoto kwa vigezo mlivyowekeana then itakuwa hivyo ikionekana haupo fit kuishi na mtoto kwa sababu fulani basi utaambiwa hivyo.

Kukaa kulalamika na kuwaza utafanya nini haisaidii chochote. Malezi ya watoto lazima yawe mutual, mkubaliane, mridhiane hata kama nyie wawili mmepishana kimahusiano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…