Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Sawa we olewa ya serikali siku utasikia kaoa msabato mwenzie ya kanisani wewe unabaki mchepuko
 
Sifa mojawapo ya mke ni kumtii mume wake,naona kabisa huyo mume wako atapata shida unapata wapii nguvu ya kutaka kumbishia hata kabla hajakuoa,,,,kikawaidaa mwanamke anatakiwa kufuata dini ya mume wake masuala ya kusemaa kila mtu afuate dini yake ni Upumbavu na huyo mwanaume atakuwa mjingaa,,,,Kama huwezii kuwa msabato basii achana nae na utakuwa bado hujafikia umri wa BORA MWANAUME YEYOTE ANAEPUMUA isitoshee wote ni wakristo sijaona ugumu uko wapii au ni ubishii wako tuu wa kutaka kumpangia mwanaume chakufanyaa,wasichana wa siku hizii mmekuwa wajinga wajinga tuu msiojielewaa huku mkijifanya mnajuaa saana halafu baadaye uje uanzee kulia unatafuta mwanaume wa kukuoa,,
 
Kuolewa ndio heshima subiri ufike miaka 35 hapo utatamani hata kizee kikuoe
 
Kwani kuna utaratibu tofauti wa ufungaji wa ndoa ukiwa dhehebu tofauti na mwenzio?

Kama ni ndiyo basi mmoja ajaribu kushuka chini
 
Hapo hamna ndoa wala usijihangaishe mnapotezeana muda tu mkuu, mwishoni huyo kijana atamuoa msabato mwenzake maana imeandikwa

2 KOR. :6:14
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?

Wewe na mwenzako mna imani tofauti wakati mwenzako anaamini siku ya ibada ni jumamosi wewe imani yako ni jpili, huyu anaamini nguruwe ni haramu wewe kwako ni ruksa tena utatamani siku uipike roast nyumbani kwenye sufuria ambalo unampikia ugali ataishia kukupiga akuue nk

Ili kuepusha hayo maandiko yanasema msifungiwe nira maana ndoa inawaunganisha wawili kuwa mmoja katika mtazamo,fikra na maamuzi sasa hii ya kwenu haitakuwa ndoa maana mtakuwa tofauti kwa kila kitu

Cha muhimu vunjeni uchumba sasa ni bora zaidi kuliko kuvunja ndoa na hata usifikirie kubadili sasa ili uolewe ili baadaye kila mtu arudi imani yake utakuwa umejitafutia shida kwenye ndoa
 
Moyo wako unasita basi KATAA NDOA maana utamtapeli tu msabato .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…