Naombeni ushauri kuhusu kubadili dhehebu ili kufunga ndoa

Nimeshaongea nae kila kitu na kwa namna niwezavyo lkn hataki..afu kinachonishàgaza sio ata mtu wa kanisani enda yake ya Mara moja au mbili kwa mwaka..Ila tu nyumban kwao baba yake ni mchungaji wa kanisa nahisi ndo Mana inakuwa hivi
Wasabato ni wabishi sana aysee,yani wabishi mnoo! Kuna jamaa yangu alikuwa na demu msabato,kipindi cha uchumba jamaa alimpa maisha sana yule demu mixer kumnunulia gari tena 2,akamfungulia mini market plus saluni za kike 2 mjini daslam hapo! Mwana akamalizia mjengo wake Geza kule fresh! Na wakati anafanya yote hayo washua wake na yule demu walikuwa wanaona na wanakenua meno tu! Kimbembe sasa jamaa akataka kuweka ndani mazima,washua na bandugu wengine wakawasha moto hatari 🔥 kwamba jamaa abadili dini,na jamaa ni RC pure mixer muhaya(kivumbi hapo) in the end ikashindikanika aysee!! Washua na bandugu wakamuamuru demu arudishe mali za jamaa,jamaa alichukua mandinga tu mini market na saluni alimuachia demu! Demu keshajaribu kujiua mara kibaoo wanamuokoa(na yeye sijui kwanini hakuwaza kubeba mimba ya mchizi) basi ndo ikaishaga hivyo,demu anawalaumu washua mpaka kesho yani! Jamaa aka move on na pisi nyingine japo hilo jambo lili mu affect sana mchizi na tulishangazwa sana na misimamo ya wale watu wasabato!! Ni watu wa ajabu sana aysee,ni kama sio wakristo vile!
(Moral of the story) bibie usitegemee huyo mkurya wa kisabato aka change maamuzi! Never on earth
Adios
 
Ongeza sita tena ifike 30 ndo utafanya maamuzi sahihi.
 
Rc hamna ndoa ya mseto Kati ya mkatoliki na msabato... Ipo Kati ya Rc na KKT, Rc na Moravian, Rc na Anglican... Lkn yy hataki anataka nifate vile anavyotaka yy
Kwenye jibu hili ndio kuna ukweli.

Usabato unapingana na RC.
Hakuna utatu mtakatifu kwenye usabato.
 
Duh so sad...
 
😂😂😂🙌
 
Msabato hana tofauti sana na mwisilamu linapokuja kwenye imani ukitaka kujua hawana tofauti ingia nae humo anavyotaka yeye utajuta ila utakuwa umechelewa!!!.
Well said
 
Sikushauri ufunge ya serikali,utawatesa sana watoto watashindwa wafate Dini ipi,ya baba au ya mama.

Ushauri wangu,sioni shida wewe kuwa msabato kama kweli unampenda mchumba wako,sioni ugumu hapo kwa sababu wote ni waabudu Kristu.
Sio kweli

Nilishawahi shuhudia ndoa Fulani

Baba muislamu mama mkristo.

Wamezaa watoto wanna wawili wa kiume na wawili wa kike.

Wakike wote walipofikisha miaka 18 walienda upande wa mama ni wakristo na wakiume walienda upande wa baba ni waislamu.

Hawakulazimishwa na mtu yeyote. Ni kwa hiyari.
 
We badili tu na ukianza kusoma Lesson utafurahia sana SABATO na hutojuta utamshukuru Mumeo
 
Kwakua ni mwanamke nakupa ushauri, badili kwa muda umsindikize kanisani kwao, ndoa ikishapita endelea kwenda parokiani kumpokea Yesu...sio dhambi..ukichelewa unawekwa pembeni anachukuliwa msabato bikra...(mm namfaham binti mmoja ana miaka 28 msabato ni bikra...wapo usikatae) Wasabato na waislam wanapenda kuoana ndani ya imani yao, ukichelewa utachacha

Wewe miaka 6 yote mnakula tunda? umeshachuja sana..ukichelewa anakuacha..olewa urudi kwa padri na pete yako...utakuja kunishukuru baadae...hizi imani ni zaidi ya unavyoijua....
 
Mimi ni mkristo nimeoa muislam alitaka kubadili ili anifuate nikakataa, tukaenda tu wilayani tukaandikisha kwenye kusaini ndoa ya wake wengi nikaona hataki, Sasa nataka nibadili dini niongeze wake mpaka mwisho wanne tazizo sina tu Hela ndo maana nmetulia naye
 
Kusema ukweli walokole wote niliwah kuhusiana Nao walinitenda sasa nimepata Mu Anglican ananipenda naMpenda tupo kwenye hatua Kama yako ila sijawah mwambia suala la kubadili dhehebu japo kuwa mama anagomagoma mimi kwenda huko

Ila mimi nime surrender
 
Dini ni utapeli ona sasa dini inataka kukukosesha mume na wote ni Watanzania ngozi nyeusi kama mkaa

Dini zimeleta chuki na mfarakano huwezi kuolewa kisa Dini ila mambo yote yapo sawa

Mababu zetu walikua wanaruhusu ndoa kama hiyo familia wanachapa kazi haswa kilimo, hawana historia ya vichaa na sio wachawi

Leo hii Dini inatutenganisha ndugu kwa ndugu [emoji24]
 
Tatz kila mtu amelelewa kwenye misingi ya dhehebu lake na usichukulie poa labda Kama hujawai kukutana na ii changamoto...na sio Kama napenda nataman iwe rhc ivyo kwangu lakn moyo ndo unanisaliti

We nae ukae nA mtu Miaka 6 then usijue nini ufanye majibu unayo bhn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…