Oa mwanamke anayemjua Mungu, anayethamini kusali si kwa mkumbo bali kwa kutoka moyoni mwake, hakikisha na wewe ni mtu wa ibada na nyote muwe kweli na hofu ya Mungu.
Kuoa ni kustaafu kujiangalia wewe, unaanza kuandaa waangalizi na warithi wako, haijalishi uliyemuoa mnaelewana au hamuelewani, chukulia hiyo ni jitihada ya shetani kutimiza mipango yake, usimpe nafasi ya kukuvuruga ukawanyima mwanga watoto wako.
Falsafa hii ni muhimu kuizingatia ili iwapo furaha kati yako na mkeo ikipungua ujue hiyo dhana ndio msingi mkuu unaopaswa kuhakikisha hauupotezi.
Usimchokoze mkeo kwa kumchanganyia mwanamke mwingine, Mungu ataondoa mkono wake ktk safari yako ya ndoa, utahangaika sana kustawisha familia yako.
Oa ukijua tabia za mkeo zitabadilika, kupunguza tatizo hilo mfundishe mapema unachopenda na usichopenda,
Kuwa mtawala mwenye hekima anayependa familia yake,
Mpe dozi mkeo ya dakika zisizopungua 10 hai 20 au zaidi kwa vyovyote isiwe chini ya dk 7, jifunze kwake anachofurahia kny tendo, ongea nae kiudadisi japo wana aibu.
Ili umtawale zaidi hakikisha akikukosea na ugomvi haujaisha hadi mnaingia kulala kamgombeze kwa kumpa dozi, story huwa zinabadilika kuanzia hapo.
Ndugu zako na wake, marafiki
na watu wengine, hawana nafasi ya kuyumbisha ndoa yako, wasikilize lkn usiwazingatie.
Maisha ya ndoa ni ulimwengu mwingine kabisa ambao ni maisha ya kuunda taifa, kwa namna yoyote kadri unavyoendelea utajua utumie njia gani kuhakikisha unawafikisha watoto wako mahala wanaweza kujitegemea bila kuonesha kuwa eewe ni muhimu kuliko mama yao, hata km mama yao ana matatizo wao watajua na wataipa kipimo hekima yako.
Zingatia:
Sala na ibada ndio mhimili mkuu wa ndoa yako. Tafuta amani na mkeo wakati wote, anaweza kukuona wewe ni kama mtoto, na wewe mchukulie hivyohivyo bila kumwonyesha waziwazi, usimdharau.
Kwa uchache, naweza kusema hayo.