Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa mkuu.usiuze ndugu kwani hao wapangaji wanakwambia hakuna thamani kwakuwa wanataka ganda la ndizi tu,wewe ndio mwenyewe na usiwasikilize wanufaika na eneo lako
Unakariri vitu.uza nyumba ya urithi ukale bata.... umejenga nyumba usijue ukiuza utapata nn jf bhana 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
🤣🤣🤣🙌wanagombana mbele ya uwanja wa nyumba yake wanataka waangukie vyombo!
Ndio salama yako.hapana
Asikutishe Mkuu mwambie kama kuna shida ya maji atafute kwingine. Binafsi nilivyohamia nikaambiwa kuna shida ya maji nilianzia Chuo cha Maji wanichimbie Kisima, nikaambiwa Milioni 7. Nikageukia Plan B, Dawasco, nikaunga Bomba kwa chini ya Laki 5, nikakomoa kwa kuweka Tanki la Lita Elfu 10. Toka nimelijaza kwa maji ya Mvua na Dawasco, mwezi wa nne huu silipi Bill ya Dawasco inasoma 0. Wekeza patakuokoa mbele ya Safari.Asante kwa ushauri huu mkuu.
Sitapauza.
Ila huyo mpangaji jamani anapaponda anasema.watu hawapati wapangaji sbb shida ya maji eti
dah pole kumbe wazazi walikufa miaka 10 iliyopita aseee pole sanaUnakariri vitu.
Nyumba nimejenga almost 10 yrs ago.
Gharama za ujenzi zimebadilika na pia nina muda sijaenda huko.Thamani ya nyumba inapanda au kushuka kwa factors nyingi.Inshort sijui hiyo nyumba ina thamani gani kwa sasa huamini vaa pajama ukalale sikulazimishi uamini
Sawa mkuu.Asikutishe Mkuu mwambie kama kuna shida ya maji atafute kwingine. Binafsi nilivyohamia nikaambiwa kuna shida ya maji nilianzia Chuo cha Maji wanichimbie Kisima, nikaambiwa Milioni 7. Nikageukia Plan B, Dawasco, nikaunga Bomba kwa chini ya Laki 5, nikakomoa kwa kuweka Tanki la Lita Elfu 10. Toka nimelijaza kwa maji ya Mvua na Dawasco, mwezi wa nne huu silipi Bill ya Dawasco inasoma 0. Wekeza patakuokoa mbele ya Safari.
Pole ndugu,biashara ya nyumba za kupangisha ni pasua kichwa sana.yaani wakati mwingine ni kama biqshara ya daladala.yaani unapewa kodi halafu kodi ikiisha mpangaji anahama unahitaji kukarabati kwa hela zaidi ya kodi aliyokulipa. Kwa jinsi nilivyokuelewa unafana na mimi,una uvivu wa kwenda kutembelea nyumba zako.wala hapo hakuna uchawi,interest yako iko chini.Hi JF.
Ndugu zangu naomba mawazo yenu.
Ni hivi, kuna nyumba iko hapo Mbezi Maramba mawili naona kama nilipoteza muda na hela zangu bure coz haina faida yeyote kwangu tokea nimeijenga.
Ilipokamilika nilimpa uncle wangu na wife wake wakae. Baada ya miaka 3 ndugu akajiongoza akaenda panga 2 rooms then akaleta mpangaji kwa 200K kwa mwezi. Ikawa ile kodi anatumia kulipia zile 2 rooms inayobaki anatumia.
Ikaenda hivyo for two years nikiwa sijui kitu coz baada ya kuwakabidhi sikuwahi tena kwenda huko hadi siku jirani mmoja kunipigia akilalamika kuhusu wapangaji wangu.Nikashangaa ikabidi niende kwa lengo lakuwatimua hao waliopangishwa bila idhini yangu.
Kufika Maramba, nilijicheka kumebadilika, kumejengwa hata njia ya kufika kwangu nimeisahau😁😁 ila nilifika nikakuta nyumba imechoka baadhi ya vioo vimevunjwa, vitasa hakuna, rangi ndo usiseme ila wapangaji walinipokea vizuri na walikua watu wastaarabu sana.
Nikajitambulisha na wakashangaa coz kwa 2 yrs wanajua ndugu yangu ndo mama mwenye nyumba wao wakaanza kulalamika kutapeliwa.
Nikawaambia hakijaharibika kitu endeleeni kukaa ila nikawaomba wanipe 300k kwa mwezi sababu nyumba imechoka coz 200K ni ndogo sana.
Hiyo 300K kwa mwezi walilipa miezi 6 tu then Covid 19 ikaja wakaomba 200k coz imempozea baba kazi, nikakubali nikiwa naplan nikaikarabati then niweke mpangaji atakayenipa hela yakuridhika.
Cha ajabu nina hiyo plan tokea enzi za Covid ila kila nikifikiria kwenda Maramba kufanya huo mchakato naona uvivu na mind you marekebisho makubwa hapo ni rangi tu na toka nilipoenda kujitambulisha sijarudi tena Maramba so mpaka leo wananipa 200K kwa mwezi ila nahisi ni ndogo sana.
Ninawaza niiuze hiyo nyumba then nikajenge kwenye moja ya plots zangu zilizoko Mtoni Kijichi.Kijichi kuna kodi nzuri.
Au niikarabati then niongeze kodi ila hapa nashindwa kuamua coz sijui soko la nyumba za kupanga likoje hapo Maramba Mawili.
So majirani zangu wa Maramba Mawili hebu niambieni eti kajumba ka 3 bedrooms,big living room,dinning,jiko,choo cha master na public,alluminium window,tiles,umeme ikiwa kwenye hali nzuri halali yake kwa mwezi ni bei gani kupangisha kwa sasa?Enzi hizo kabla wakati nampatia uncle wangu alipatikana mpangaji wa 350K kwa mwezi kwa kila miezi 4.
Na je nikisema niuze nitapata kiasi gani eti majirani zangu wapendwa(Kwa kukadiria)
Natanguliza shukrani zangu Majirani zangu wapendwa.Sisi ni ndugu tusaidiane🙏🙏
Hapo kuna mradi wa mwendokasi unapitaNataka karibu na askari monument mkuu