Naombeni ushauri kuhusu nyumba yangu niliyoijenga Maramba Mawili

Mkuu pale makuti kupo poa Sana ipo karibu Na Ile shelly ya Olympic.

Nilipita pale wakati naenda Tabata
Hiyo shell siijui mkuu nina muda sijafika huko ila naenda huko soon
 
Coz. Coz coz,namashaka mtu awe na shumba Malamba mawili halafu awe anaandika coz coz kama kiform two🀣🀣chai
coz is coz mkuu but chillax coz life is short😁
 
usiuze ndugu kwani hao wapangaji wanakwambia hakuna thamani kwakuwa wanataka ganda la ndizi tu,wewe ndio mwenyewe na usiwasikilize wanufaika na eneo lako
Kabisa mkuu.
Nitafanya jambo soon.
Hali ngumu ni ujinga kuacha hata mia tano ipotee kizembe
 
uza nyumba ya urithi ukale bata.... umejenga nyumba usijue ukiuza utapata nn jf bhana 🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Unakariri vitu.
Nyumba nimejenga almost 10 yrs ago.
Gharama za ujenzi zimebadilika na pia nina muda sijaenda huko.Thamani ya nyumba inapanda au kushuka kwa factors nyingi.Inshort sijui hiyo nyumba ina thamani gani kwa sasa huamini vaa pajama ukalale sikulazimishi uamini
 
Hivi maramba mawili hilo neno MARAMBA maana yake nini katika jina silipendi ni hilo
Niliambiwaga maana yake ila nimesahau.Nahisi maramba maana yake ni mabwawa
 
Asante kwa ushauri huu mkuu.
Sitapauza.
Ila huyo mpangaji jamani anapaponda anasema.watu hawapati wapangaji sbb shida ya maji eti
Asikutishe Mkuu mwambie kama kuna shida ya maji atafute kwingine. Binafsi nilivyohamia nikaambiwa kuna shida ya maji nilianzia Chuo cha Maji wanichimbie Kisima, nikaambiwa Milioni 7. Nikageukia Plan B, Dawasco, nikaunga Bomba kwa chini ya Laki 5, nikakomoa kwa kuweka Tanki la Lita Elfu 10. Toka nimelijaza kwa maji ya Mvua na Dawasco, mwezi wa nne huu silipi Bill ya Dawasco inasoma 0. Wekeza patakuokoa mbele ya Safari.
 
dah pole kumbe wazazi walikufa miaka 10 iliyopita aseee pole sana
 
Sawa mkuu.
Mimi nilijenga kisima cha kuvuna maji ya mvua.Wananunua ya kupikia tu.
 
Mbona mnasema ni Chai au wivu unawasumbua....πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒyani mtafanya watu washindwe kuleta vitu muwashauri...
 
Pole ndugu,biashara ya nyumba za kupangisha ni pasua kichwa sana.yaani wakati mwingine ni kama biqshara ya daladala.yaani unapewa kodi halafu kodi ikiisha mpangaji anahama unahitaji kukarabati kwa hela zaidi ya kodi aliyokulipa. Kwa jinsi nilivyokuelewa unafana na mimi,una uvivu wa kwenda kutembelea nyumba zako.wala hapo hakuna uchawi,interest yako iko chini.

Biashara ya nyumba inataka mmiliki mkorofi ndiyo utaiona hela,vinginevyo sounds ni nyingi sana na uhabifu ni mkubwa sana.Wakati mwingine unajenga kwa sababu ya watoto wawe na mahali pa kuanzia ila siyo biashara kwa kweli.Labda ujenge vinyumba vya bei vya bei rahisi huko uswahili uoate elf 30 kwa room.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…