Naombeni ushauri: Mke wangu amejua kuwa nina mtoto kwa mwanamke mwingine

Mkuu kwa comment hii unaweza kumuolea mke wa pili kabla hajamaliza kufungasha virago.

Style ya Kanye West, kabla talaka haijakamilika ushatoka na model mpya mkali zaidi magazetini.
Huwa nawaambia mabinti zangu, pamoja na kwamba wanawake sio watu wa kuwachukulia umakini sana katika kila jambo lakini haina maana kwamba kila ujinga ni wa kuwachekea.

Ndoa ni zaidi ya kulalana kitandani, sio jambo la mzaha mzaha tu. Fikiria mkeo wa ndoa anakutishia eti "naondoka narudi nyumbani kwa wazazi wangu", mke wa ndoa anakuambia hivo na mdomo kauvuta ~ namwambia nenda lakini hakikisha unakaa na hao wazazi wako hadi nitakapokufuata [emoji16][emoji16]
 
Saa zote kumbe ulikuwa hujatoa ushauri??
 
Acha uchonganishi wewe, atubu kwa lipi? kama kabaka sawa au kazzaa na mke wa mtu
 
Kugawana mali ni haki yake, hawezi ondoka mtupu kwa muda aliokaa Kuna vitu amechangia wanaume wengi mnapenda mkiachana na mwanamke basi asipate popote pa kushika ndo furaha yenu
Sio furaha yangu kuona wanandoa wanaachana. Sasa kwanini aondoke wakati ana watoto wadogo mmoja miaka 4 na mwingine mwaka 1.

Wagawane mali akaishi mwenyewe atoke na waume za watu au viserengeti boys watoto wake waishi kwa tabu. Kisa tu mtoto mmoja wa nje?

Kugawana mali ni haki yake ila kwanini wafikie kuvunja ndoa.
 
Ukisema .unaonekana una uzoefu wa kuchepuka.me siondoki
 
Muache asepe kwani ndgu yako,huyo mpita nja ila mtoto atabaki ndgu yako milele.
 
Ndo hivo mkuu .Mimi namchukua tu mtoto akae na wenzake maisha yaendelee.ukiondoka unamfaidisha Nani zaidi ya kuleta maafa kwa wanao?
Comment hii inaonyesha Ni jins gani ulivyo mwanamke MATURED. Bravo[emoji106]
 
Inanishangaza.....
 
Kuandika huku jf flani Malaya hakumfanyi kuwa Malaya .uzoefu wa kuandika bila research Ni ziro tu.
Kila mtu ana style zake za kuishi
Kama hujui stress inaua basi chagua stress.


Nisome vizuri tena utaona sijaku attack wewe personal kuwa Malaya isipokuwa kama uta qualify kwenye hizo tabia anajua ni Mungu na wewe binafsi.

Niko makini sana na uandishi wangu always.

Nimejifunza tangu Mdogo namna ya uandishi wa mahusiano na mawasiliano.

Utaona huwa napenda kutumia nafsi ya tatu ktk kuelezea na si nafsi ya kwanza wala ya pili labda ibidi kufanya hivyo.

Kwa hiyo soma tena kisha jipime mwenyewe.
 
Kuihimili hili zigo inataka moyo sana
👉Umri mkubwa ndo wanaweza hili
👉Kama ke nae ashachepuka nje ya mumewe ama kuzaa nje akiwa kaolewa
👉Una roho mtakatifu

Vinginevyo hapo pagumu Sana sitaki hata kupawazia
 
Hii ishu upande wa pili ni ruksa hata wake wa nne.

Ila sasa nyie wenzetu mnatupinga na sheria zetu

Cha ajabu nyie mnafanya kimyakimya

Fanyeni marekebisho
Kuliko ivi mnavo fanya
Mnawatesa sana wamama
 
Ushauri bora muulize huyo Mkeo....,

Sababu akikubaliana na wewe kila kitu umemaliza; Anyway wanasema Zege ukishalikoroga halirudi tena kuwa sementi....,

kwahio kuwa mpole tu vumilia masimango na lawama kila ukifanya kosa dogo kwa muhusika kukumbushia ulivyofanya...
 
Ushauri mke wangu anataka kuondoka kisa nimezalia kwa mwanamke mwingine .Sasa tumebahatika kujenga kibanda na tuna duka sasa anataka tugawame.
Huyu anataka mali amepata sababu ya kusema,hakuna mkamilifu hapa duniani mngezungumza na kuyamaliza ila kama anataka mgawane mali basi ni mwenye tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…