Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Wanaume wengine bwana; kwa hiyo wewe ulikuwa unakula tu mzigo bila kujua kuwa Mimba itaingia?
Kwa nini hukujadili na mkeo mkapata ushauri wa namna ya kuzuia Mimba hadi mtoto akue?
Hata hivyo sio mbaya sana kwani mkeo anaweza kuendelea kunyonyesha kwa miezi mingine hata 5 hivi ambapo dogo atakaribia miaka miwili ambayo ndio umri sahihi unatakiwa kumuachisha kunyonya.
Sawa Mkuu nimekulewa Sana be blessed 🙏🙌🙌🙌
 
Uwepo wangu sio muhimu mkuu tupo jf kuburudika na kujifunza
Kuanzia kesho ntakuwa mute nikaanze majukumu yangu nilikuwa Nina likizo ya wiki kwa ajili ya kuaga.
Respect sana Half american utamsalimia Shunie mwambie nishaondoka nimemuachia jf yake[emoji16]
[emoji1787] Ila nitakumiss ujue nakuombea sana unapoenda uende salama urudi salama
 
Habari muda huu Wana JF poleni na majukumu mbalimbali na ramdhani Kareem kwa ndugu zangu waislamu.

Juzi siku ya jumamosi mke wangu alianza kutapika uku akilalamika anajisikia uchovu, leo Imebidi nimpeleke hospital kwa ajili ya vipimo Mana Hali iliendelea vilevile, baada ya vipimo imegundulika ana mimba ya mwezi mmoja hiyo taarifa imenishtua Sana Ila nilivyomuangalia mama N yupo kawaida nahisi alishajigundua Hali yake tokea muda.

Njiani wakati tunarudi hakuna mtu aliomuongelesha mwezake, kitu kinachonipa mawazo tuna mtoto mdogo ana mwaka na miezi 4 na mke wangu mimba ikifika miezi 5 ni kuumwa kila siku je mtoto atapata malezi Bora au nimpeleke kwa Bibi yake.

Niliona dalili kitu kidogo akikosea mtoto anamkaripia wakati hakuwa hivo nyuma.

Naombeni Ushauri Wana JamiiForums.

Ushauri kwamba uitoe au? Hakuna namna, hapo ni mkeo alee mimba tu, ushauri ni kwamba: Yanawezekana bila shida. . Mkiwa mnafanya mapenzi kunakuwaga na matokeo, ndo hayo sasa.
 
Back
Top Bottom