Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Muda mwingine mnajitengenezea maradhi wenyewe
Eti akifika miezi mitano lazima mimba imsumbue,
Nani kasema mimba zinafanana
 
Habari muda huu Wana JF poleni na majukumu mbalimbali na ramdhani Kareem kwa ndugu zangu waislamu.

Juzi siku ya jumamosi mke wangu alianza kutapika uku akilalamika anajisikia uchovu, leo Imebidi nimpeleke hospital kwa ajili ya vipimo Mana Hali iliendelea vilevile, baada ya vipimo imegundulika ana mimba ya mwezi mmoja hiyo taarifa imenishtua Sana Ila nilivyomuangalia mama N yupo kawaida nahisi alishajigundua Hali yake tokea muda.

Njiani wakati tunarudi hakuna mtu aliomuongelesha mwezake, kitu kinachonipa mawazo tuna mtoto mdogo ana mwaka na miezi 4 na mke wangu mimba ikifika miezi 5 ni kuumwa kila siku je mtoto atapata malezi Bora au nimpeleke kwa Bibi yake.

Niliona dalili kitu kidogo akikosea mtoto anamkaripia wakati hakuwa hivo nyuma.

Naombeni Ushauri Wana JamiiForums.

Unataka tukushauri nini

Zaeni na mlee watoto wote wawili, tena wewe ndio umsaidie kwa upendo. Huko kwa bibi mnampelekea mtoto kumtesa bibi na kumtesa mtoto kwa kumnyima haki ya kuwa na wazazi wake.

Mkijua kuingiza mimba mjue kuitunza na kulea kinachozaliwa
 
Thread ya ngapi hiii bora uondoke tu
Ujue tangu jf waanzishe utaratibu wa kutoa zawadi kwa members wenye michango mikubwa kwenye majukwaa mbalimbali wameibuka wajinga wajinga wengi sana kulazimisha umaarufu humu, akiwemo mtoa mada
 
Kwa kuuliza swali la kitoto kama hili,basi ni wazi kabisa kua uliwahi kuoa kabla akili yako haijakomaa.
 
Utaacha kuwa na mawazo wakati mtoto sio wako😂😂😂😂 alafu iweje mtu akiwa na mimba ya miezi 5 awe anaumwa kila siku au lishe ndani ya familia ni duni? Nikisema duni simaanishi kwamba huna pesa ila unazitumiaje kwwnye milo ya familia. Jipange usije ukawa chizi
 
Back
Top Bottom