Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Naombeni ushauri, Mke wangu ana mimba nyingine

Baadhi ya wanaume hawatoi ushirikiano kabisa kwenye swala la uzazi wa mpango kabla haya hayajatokea.... Then yakitokea wanaleta uzi JF🤭🧐😴
 
Mimi na kaka yangu tunapishana miaka miwili. Sasa huyo mtoto ana mwaka na miezi minne jumlisha miezi nane ya mimba atakuwa tayari na miaka miwili na miezi kadhaa. Lea mimba mkuu.
 
Habari muda huu Wana Jf poleni na majukumu mbalimbali na ramdhani Kareem kwa ndugu zangu waislamu.

Juzi siku ya jumamosi mke wangu alianza kutapika uku akilalamika anajisikia uchovu,leo Imebidi nimpeleke hospital kwa ajili ya vipimo Mana Hali iliendelea vilevile.baada ya vipimo imegundulika ana mimba ya mwezi mmoja hiyo taarifa imenishtua Sana Ila nilivyomuangalia mama N yupo kawaida nahisi alishajigundua Hali yake tokea muda.

Njiani wakati tunarudi hakuna mtu aliomuongelesha mwezake.
kitu kinacho Nipa mawazo tuna mtoto mdogo ana mwaka na miezi 4 na mke wangu mimba ikifika miezi 5 ni kuumwa kila siku je mtoto atapata malezi Bora au nimpeleke kwa Bibi yake.

Niliona dalili kitu kidogo akikosea mtoto anamkaripia wakati hakuwa hivo nyuma.

naombeni Ushauri Wana Jamii forum.
Wanaume wengine bwana; kwa hiyo wewe ulikuwa unakula tu mzigo bila kujua kuwa Mimba itaingia?
Kwa nini hukujadili na mkeo mkapata ushauri wa namna ya kuzuia Mimba hadi mtoto akue?
Hata hivyo sio mbaya sana kwani mkeo anaweza kuendelea kunyonyesha kwa miezi mingine hata 5 hivi ambapo dogo atakaribia miaka miwili ambayo ndio umri sahihi unatakiwa kumuachisha kunyonya.
 
Back
Top Bottom