Naombeni ushauri, mtoto wangu ana tapika na kuanguka

Nenda hospital kubwa ungesema upo mkoa gani , ungesaidiwa uanze na hospital ipi lakini muhimu kumuona daktari bingwa wa watoto fanya hili mapema
 
Asante sana mkuu
 
Pole sana kwa kuuguliwa. Ushauri utakaopata hapa sana sana ni kumpeleka hospital. Unasema kuwa umempeleka zahanati na kupewa dawa za malaria. Sidhani kama huu ugonjwa zahanati wanaweza kuushughulikia. Inaoneka ana tatizo linalohitaji dakta mtalaam, hasa wa mambo ya watoto. Na hata kama ukienda hospital moja asipopona rudi tena na zaidi jaribu kubadilisha hospital. Kutegemeana na mkoa ulipo, nenda hospital kubwa.
 
Pole mkuu, pia angalia lishe ya mtoto angalau awe na uzito sahihi kwa umri wake!
Kwa experience yangu ya umama watoto wenye uzito mdogo wakipatwa na ugonjwa homa huwa inakua kali sana kupelekea degedege tofauti na wengine
Nb. Mimi sio daktari hiyo ni observation yangu tu.
 
Matibabu Bora ni Yale yamayo fanywa pande zote mbili , hospital na kwa waganga njaa.
Huwez kujua labda karogwa huyo
 
Kutapika plus Kuanguka" ????😳😳😳 Embu peleka mtoto kwenye high facility RRH
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…