Naombeni ushauri! Mwanangu wa kike kaniambia Mambo yaliyonichanganya sana

Naombeni ushauri! Mwanangu wa kike kaniambia Mambo yaliyonichanganya sana

Naombeni ushauri, namuokoa vipi mwanangu wa miaka minne na kumkinga katika Hali hiii. Ni hivi, Leo nilikuwa nyumbani, na toka asubuhi nilikuwa nae nikicheza nae .

Sasa katika ongea ongea kaniambia Jambo lililonishtua kidogo. Ameniambia watoto wadogo wawili wa pale mtaani wamedakana. Na nilipouuliza kudakana ndio Nini akasema walienda kwenye migomba wakavua nguo na kudakana.

Kwa jinsi alivyoongea,Mimi nimeelewa kuwa hao watoto walifanya mapenzi japo yeye anasema walidakana. Haraka haraka nimejua kuwa lazima Kuna mtu kamwambia kitendo kile ni kudakana .

Kinachonitisha zaidi watoto anaosema wamedakana ni watoto wadogo wachekechea.

Kwa umri wake kuanza kuongea au kusikia Mambo Kama hayo naona Kama sio sawa.

Naombeni ushauri katika mazingira Kama haya namsaidia vipi mwanangu , na pili namweka vipi mbali na hao watoto wengine pasipo kuleta athari. Japo najua kumtenga sio dawa, maana hawezi kuishi ndani peke yake. Tushauriane katika malezi,kwenye Jambo Kama hili unafanyaje kumuokoa mwanao wa kike.
Sisi wakati ni wadogo tulikuwa tunauliza hivi mtoto anazilowajie unajibiwa eti anatoka kwenye mapaja unatafakari hupati jibui sahihi muda unavyoenda unasahau kuulizi tena ama kufuatilia hahaha utoto bana natamani kurudi utotoni ili nipange upya , (back to the future) vijana wa kizazi tafuteni move,(filamu) inayoitwa back the future
 
Back
Top Bottom