Malezi siku hizi ni changamoto sana watoto wana too much information.Naombeni ushauri, namuokoa vipi mwanangu wa miaka minne na kumkinga katika Hali hiii. Ni hivi, Leo nilikuwa nyumbani, na toka asubuhi nilikuwa nae nikicheza nae .
Sasa katika ongea ongea kaniambia Jambo lililonishtua kidogo. Ameniambia watoto wadogo wawili wa pale mtaani wamedakana. Na nilipouuliza kudakana ndio Nini akasema walienda kwenye migomba wakavua nguo na kudakana.
Kwa jinsi alivyoongea,Mimi nimeelewa kuwa hao watoto walifanya mapenzi japo yeye anasema walidakana. Haraka haraka nimejua kuwa lazima Kuna mtu kamwambia kitendo kile ni kudakana .
Kinachonitisha zaidi watoto anaosema wamedakana ni watoto wadogo wachekechea.
Kwa umri wake kuanza kuongea au kusikia Mambo Kama hayo naona Kama sio sawa.
Naombeni ushauri katika mazingira Kama haya namsaidia vipi mwanangu , na pili namweka vipi mbali na hao watoto wengine pasipo kuleta athari. Japo najua kumtenga sio dawa, maana hawezi kuishi ndani peke yake. Tushauriane katika malezi,kwenye Jambo Kama hili unafanyaje kumuokoa mwanao wa kike.
Mimi watoto wangu watu wengne wanadai nawafungia sana ila sina namna ni shule, getin wachezee ndani.
Hao wanaonisema chini kwa chini siku moja nimekuta wanagombana mmoja akidai mtoto wa mwenzake kambaka mtoto wake. Na mama wa mtoto anayedaiwa kubaka akasema eeh mwanangi kidume. Aliyebakwa ni la nne aliyebaka la sita.