Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Mwache mama yako apate raha za maisha wewe!! Huwezi kumtolea maamuzi mama yako!
 
Acheni roho mbaya aisee ungekuwa wewe kibabu watu wanakufanyia fitini mitandaoni usimpate mywako ungefurahiiiii???kila mtu anapenda vitamu.
Roho mbaya hiyo kwio,.?? Kwani anayeoa ni mwanaume au mwanamke..??
 
Hili swala lilishaahi kumkuta baba wa rafiki yangu aisee ilikuwa msala sana
 
Mkuu kwa umri wa mama yako hapaswi kuolewa tena pia sio busta kwa umri wake amlete marioo aje kuishi nae kwenye nyumba ya mzee wako.me baba yangu alifari mwaka 2006 kamuacha mama kwa sasa ana umri wa miaka 65 sijawai kumsikia akisema anataka kuolewa na siku nikimsikia sijui itakuwaje maana ajali kwa kila kitu kikubwa apo nikusimama kiume kama anataka kuolewa basi aende kwa huyo mwanaume na sio uyo marioo aje kwenye boma lingine wakati nae anaboma lake iyo ni mila ya wapi mkuu
 
Hapana mzuie. Ila daah...! Kuna akina mama nao ni noma. Miaka 68 tamaa gani hiyo?.
Hapo anajitafutia kufa haraka tu.

Nina mamaangu mkubwa tumemzika tarehe 31/12/21. Mumewe ambae alikuwa babangu alifariki mwaka 79,hapo mama mkubwa akiwa na umri wa miaka 57. Tangia hapo bimkubwa sikuwahi kumuona anahangaika na mwanaume. Tangia afe mumewe hajaonekana na mwanaume.

Na hiyo ilimfanya adumu muda mrefu. Mpaka anafariki tarehe 27/12/21 alikuwa katimiza miaka 99. Mimi ndie nilikuwa namtunza kwa kila kitu. Katika maisha yake yote hakuwahi kuugua mpaka kulazwa.
 
Alikuwa naye huyo babu, sio rahisi miezi 8 tayari mchakato wa ndoa duu! Walio na umri mdogo wenyewe waume zao huwatelekeza.lakini hawa hangaiki kihivyo.
 
Hicho kizee ni cha kukikamata na kukikata mapu.mbu..maana kishatumia ndumba hapo..
 
Wewe uliweka maisha standard wazee walikuwa wanayamezea mate, kwahiyo kijana unalo, nakushauri tu kuwa hisia kuzicontrol ni ngumu inaonekana mama Yako bado anataka asukumiwe mzigo na huyo Mzee mwenzake anatakafuta unafuu wa maisha kwasababu anaona kitonga kipo nakushauri kama ulishamwelewesha mama Yako na haelewi achana nae focus kwenye mambo Yako na familia Yako
 

Nakushauri nenda kwa mwanasaikolojia kama Chris Mauki au Dr. Elly wakupe ushauri wewe kisha wampe na Bi Mkubwa ushauri kwa kuolewa au kutoolewa.
 
Alikuwa naye huyo babu, sio rahisi miezi 8 tayari mchakato wa ndoa duu! Walio na umri mdogo wenyewe waume zao huwatelekeza.lakini hawa hangaiki kihivyo.
Usikute ndio baba wa mwandishi wa huu Uzi.
Wakimtubua mama wataletewa na Siri zisizofaa.
Waende naye taratibu.
Kata mrija wa mafuta tu.
Tunaamini muoaji lazima awe mtafutaji
 
Ukisoma michango ya baadhi ya wachangiaji, mara moja utabaini tatizo kubwa katika jamii yetu: uduni wa maarifa ya na stadi za maisha miongoni mwa wengi wetu; na udhaifu katika stadi za mawasiliano hasa kwa njia za maandishi. Hoja iliyoletwa ni nzito na kwa kweli inahitaji akili zilizotulia kutafuta ufumbuzi. Shukrani kwa waungwana wote wanaotoa michango yenye tija. Na wale wengine wanaofanya mizaha au wenye maarifa duni waone busara katika kukaa kimya, kwa maana, mjinga akivumilia kukaa kimya hudhaniwa ni mwerevu mpaka pale atakapofungua kinywa chake.
 
Usikute ndio baba wa mwandishi wa huu Uzi.
Wakimtubua mama wataletewa na Siri zisizofaa.
Waende naye taratibu.
Kata mrija wa mafuta tu.
Tunaamini muoaji lazima awe mtafutaji
Haa haa haa haa mwee jamani
 
Kwa hiyo ni heshima kutoolewa ila awe anamegwa kisela? Nimeshuhudia wamama wengi wajane hawaolewi ila wanamegwa kisela! Hiyo ni heshima kwa familia au uchafu? Kwa mimi kama anatulia basi atulie ukweli wa kutulia, ila kama bado anahitaji faraja ya mwanaume ni kheri akaolewa
 
mZee mam ako Ni kabila gani ..lkn kwann awazalilishe HV hpn Wal usimlete nyumbani kwako ila naona pengine ameona amuweke mzee mtu mzima wazaidiana. Hata Kaz ndogondgo hapo kwake muache tu
 
Kwa thread hii nimeanza kuelewa kwanini jamaa yule alisema MWANAMKE SIO WA KUMWONEA HURUMA.
Mtu una miaka 68 na ni miezi 8 tu tangu mumeo aage Dunia?!
Kweli Mke sio ndugu yako,ndugu zako ni watoto wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…