Naombeni ushauri: Nataka kumzuia mama yangu asiolewe tena baada ya baba kufariki

Habari ndugu zangu. Naombeni ushauri wenu juu ya mada tajwa.

Mzee wetu amefariki miezi 8 iliyopita baada ya maisha yake yote kuwa katika ndoa na mama yetu. Mama Sasa ana umri wa miaka 68. Kwa kipindi chote tangu sisi watoto wake tuanze kujitegemea tumekuwa tukijitahidi kuwawekea mazingira mazuri ya wazee wetu. Pamoja na kuwajengea nyumba yenye hadhi na ya kisasa lakini tumehakikisha wazee wetu wanaishi maisha standard kuanzia chakula na mahitaji yote kiasi kwamba familia ya mzee wetu imetazamwa kama familia yenye nafuu pale kijijini.

Juzi ndugu zangu waliopo kijijni wamenitaarifu kwamba kajitokeza mzee anasema anataka kumuoa bi mkubwa. Nikauliza akishamuoa ataondokanae kwa maana bi mkubwa atahama mji tuliomjengea na mzee? Wakaniambia hapana inavyoonyesha huyu mzee kafuata maisha mseleleko.

Binafsi nimejiuliza je ni sahihi mama alete mwanaume kwenye kitanda alicholala na mzee wetu? Je ni kweli nyumba tuliowajengea wazee wetu mama atumie kuishi na mzee mwingine? Alifanyalo mama sio kutufedhehesha sisi watoto tunaohakikisha anapatiwa chochote akitakacho?

Uamuzi wangu nimepanga kuvuruga mpango wa bi mkubwa. Nataka nimwite nimuombe nije niishi nae mjini kwa maisha yake yote ili nizuie mipango yake na akikataa nimepanga sitomuhudumia chochote maana Mimi ndie mwanawe mpendwa.
Je ndugu uamuzi wangu huu nitakuwa namkosea mama yangu? Au nimwachie tu ahangaike na maisha yake? Kinachoumiza mzee muoaji mwenyewe kachoka mno hata ndala anazovaa ukute zina matundu nusu anagusa ardhi nusu malapa. Naona kama bi mkubwa atatuongezea mzigo wa kuangalia watu wawili kwa maana akibaki mwenyewe inakuwa rahisi hata kumchukua wakati wowote. Ushauri wenu

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Acha iyo tabia ya kuingilia mahusiano ya watu wazima, tena ukute Hilo lizee ndo babaako mzazi.
 
Ndugu hujaweza na hutoweza kumtimizia haja za moyo wake, wewe mpokee huyo baba kama mama karidhika nae! na hata usipo-supply huduma ya chakula huyo bi mkubwa atakuwa na raha sana na huyo unaemwita mzee, nakwambia mama ndie atahangaika ili huyu mrithi ale na amle vyema!!
 
Duh, huyo mzee inaonekana ndio waleeee ganda la ndizi tangu ujana wake, afu' anajua sound kinoma kampigisha bi mkubwa kaingia line woiii... in short huyo babu ana mipango yake hapo...
Alikua mpango wake wa kando,sasa wanahalalisha
 
Ndugu hujaweza na hutoweza kumtimizia haja za moyo wake, wewe mpokee huyo baba kama mama karidhika nae! na hata usipo-supply huduma ya chakula huyo bi mkubwa atakuwa na raha sana na huyo unaemwita mzee, nakwambia mama ndie atahangaika ili huyu mrithi ale na amle vyema!!
Kuna umri ukifika mzee anakuwa kama mtoto, kama mama atamudu kumlea huyo mzee mwenyewe, na amlee ila sisi hapana. Ukioa sharti uwe na mji wako wa kumuweka mkeo. Mzee amchukue mkewe wakaishi kwake!

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Kwa ufupi kaeni vikao nyie watoto wake mfanye tafakuri lkn pia kumbuka mama yenu anaitaji kuwa na furaha katika maisha yake yaliyobaki, inawezekana pia bado anataka kunyanduliwa kumbuka kuna wanawake iyo kitu wanaifurahia mpaka kwenye 80s kulingana na makuzi yake na hormone then muone cha kufanya. Lakini the bottom line uyo muoaji (Baba yenu wa kambo) hasije kwenye nyumba yenu.
 
pole mkuu sisi katika UISLAM mtoto wa kiume tunaruhusiwa hata kuozesha MAMAAKO

ni kweli kwa umri wake na ukizingatia mumewe amefariki muda si mrefu ilipaswa apumzike

lkn wewe inaonesha wasiwasi wako sio mama ni umasikini wa huyo mzee

nikuulize angetokea mtu mwenye pesa na kujiweza mwenye magari majumba na biashara zake je ungekubari aolewe ?

Vipi mama akihama dini?
Kinachomuuma kijana ni mali za kurithi.
Maoni uangu: Usimpangie mama yako ni lini mahitaji yake ya kibailojia yanapaswa kuisha, kama una mke muache mkeo na wewe ubaki mpweke kama mama yako halafu mtaongea lugha 1.
Siku akihitaji mwanaume utamhudumia?
NB mama anahitaji mwenza sio tu kwa ajili ya tendo la ndoa bali kampani walale wote, wale wote n.k kikubwa tu asilete mzee wakutafuna mali rafu ila kam ni misosi wacha wale tafuta zako na mkeo.
 
Hamchukii huyo mzee sema anachukia mamaake kuolewa na mtu ambaye hana hela ndala zimetoboka.
Hiyo pia ni sababu, ni kweli na yupo sahihi. Ataongeza mzigo huyo mzee, je, hana watoto? Hajachukia kuolewa na mzee, ila anataka mzee ampeleke mkewe kwake, sio kung'ang'ana kwenye nyumba ya marehemu. Kiheshima si nzuri na haipendezi. Ila kama mzee anang'ang'ania kukaa kwa mwanamke, ni bora achukue maamuzi magumu akate huduma kwa mama au aizuie ndoa hiyo kibabe.

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Kuna umri ukifika mzee anakuwa kama mtoto, kama mama atamudu kumlea huyo mzee mwenyewe, na amlee ila sisi hapana. Ukioa sharti uwe na mji wako wa kumuweka mkeo. Mzee amchukue mkewe wakaishi kwake!

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
Hakuna umri wa kuacha kuhudumia mwili wa ndani! Mwache mama usimnyanyase kwa haya mahitaji umpayo, mpokee huyo baba mama aishi zaidi!!
 
Vipi mama akihama dini?
Kinachomuuma kijana ni mali za kurithi.
Maoni uangu: Usimpangie mama yako ni lini mahitaji yake ya kibailojia yanapaswa kuisha, kama una mke muache mkeo na wewe ubaki mpweke kama mama yako halafu mtaongea lugha 1.
Siku akihitaji mwanaume utamhudumia?
NB mama anahitaji mwenza sio tu kwa ajili ya tendo la ndoa bali kampani walale wote, wale wote n.k kikubwa tu asilete mzee wakutafuna mali rafu ila kam ni misosi wacha wale tafuta zako na mkeo.
At least umemshauri safi, mzee akae kwake na mkewe, sio nyumbani kwa mwanamke. Na umri huo hana watoto huyo mzee?

Sent from my A50s using JamiiForums mobile app
 
Chukua Huu Ushauri Wangu Halafu Umwambie Wazi
Mtu Umri Miaka 68 Ndoa Gani Hiyo
Akilazimisha Kuolewa Mwambie Hatapata Kumi Nyekundu

Huyo Muoaji Akikaa Kwenye Mji Wenu Mtaanza Kugombana Daily

Wazee Wetu Ukimuita Aje Akae Mjini Atagoma
Ila Mwambie Yote Unayotaka Kutekeleza Endapo Ataolewa
 
Si kugombana tu, kuna kuuana pia kisa mali n.k! Huyo mzee ana watoto wakubwa(huenda), ndugi n.k, sasa wakiishi sana huoni italeta utata wa mali? Suala ni kuwa, mzee watoto wake wapo wapi? Lazima uone aibu kuhudumiwa na watoto wa mwanaume mwenzio, na huku unao wako. Huyo mzee hatakiwi kuchekewa.

Back
Top Bottom