Naombeni ushauri nina mtaji wa 50,000 (Shilingi elfu hamsini)

Naombeni ushauri nina mtaji wa 50,000 (Shilingi elfu hamsini)

min -me
Soma hapa ,na usitoe maoni ukiwa na vant kichwani
Nimetoa maoni , kama mpango wa mda mrefu na sio kuwinda 2000, kama anawinda hiyo 2000 atumie hiyo 50k kama nauli aje afagie mabanda ya mifugo nitamlipa 3000 kwa siku.

Umeshaelewa?
 
Unaweza kuuza mayai ya kuchemsha, mihogo, matunda yaliyokatwa, au maji sehemu zenye watu wengi kama vituo vya daladala, masokoni au karibu na vyuo.

Kwa huo mtaji unatosha kabisa , kikubwa uwe na nidhamu, usije kuula na huo mtaji tena.
 
Nimetoa maoni , kama mpango wa mda mrefu na sio kuwinda 2000, kama anawinda hiyo 2000 atumie hiyo 50k kama nauli aje afagie mabanda ya mifugo nitamlipa 3000 kwa siku.

Umeshaelewa?
50k mpango wa mda mrefu?
Mzee mtu kama huyu anatakiwa kusurvive maana graph yake inashuka kwa speed kubwa sana
 
Ondoa aibu kabisa,pita kariakoo au posta maduka ya waarabu ya hard ware na machine tools.
Fika pale with full of confidence waambie unateseka sana na maisha ,mfukoni una 50k na ndio life line Yako hiyo.

Waombe mzani wa kupima uzito watu.
Hapa hukosi 10k per day plus keep change kama zote
Trust me ukipita maduka matatu hukosi kusaidiwa duka Moja.
 
Tafuta kimeza kisha nunua vinywaji vikali mfano konyagi kubwa moja na K-vant na vikombe vya take away vile kisha weka nje kidogo ya mabaa makubwa. Uza cha kupima

Usisahau kuweka pakti za sigara.
 
Nunua ungo, karanga, pakti za sigara

Tembeza stand mida ya jioni na asubuhi ndani ya wiki 2 mtaji unarudi, ukipenda kuendelea sawa
 
Samahani wakubwa nimeuza vitu vyangu kadhaa nimepata Shilingi elfu hamsini,
nahitaji hii Hela isipotee maana sijui nitapata lini Tena.

Naombeni wazo la shughuli ya kufanya Kwa kutumia kiasi hiki Cha Pesa na nipate faida.

Niweze kuweka akiba ya 2,500 Kila siku

Jinsia mwanaume miaka 28 Dar es salaam
Natanguliza shukrani za dhati Kwa maoni mtakayotoa
Mkuu nunua mihogo ile yenye unga kaanga uza kisasa ilo 50k latosha, au uwe unafunga vifurushi unaweka kwenye besenu unauza pale ubungo mataaa unazungusha hiyo hela
 
Samahani wakubwa nimeuza vitu vyangu kadhaa nimepata Shilingi elfu hamsini,
nahitaji hii Hela isipotee maana sijui nitapata lini Tena.

Naombeni wazo la shughuli ya kufanya Kwa kutumia kiasi hiki Cha Pesa na nipate faida.

Niweze kuweka akiba ya 2,500 Kila siku

Jinsia mwanaume miaka 28 Dar es salaam
Natanguliza shukrani za dhati Kwa maoni mtakayotoa
Njoo uzi wa wakamaria ukamate odds 2 kwa siku
 
Tafuta kimeza kisha nunua vinywaji vikali mfano konyagi kubwa moja na K-vant na vikombe vya take away vile kisha weka nje kidogo ya mabaa makubwa. Uza cha kupima

Usisahau kuweka pakti za sigara.
Kwamba hy huduma itakuwa haipo kwenye hizo bar hadi kufanya wanywaji kununua nje?
 
Nunua mitetea miwili na jogoo mmoja wa saizi ya kati fuga, watage halafu wataamishie , weka mayai 15 kwa 15 kwa kila mtetea , watoto utakaowapata wafuge
Anaishi Dar, pengine amepanga chumba kimoja kwenye zile nyumba 'face me I face you', hao kuku atawafugia wapi? Hao kuku watahitaji chakula, chanjo n.k...hayo yote atayafanya kwa hiyohiyo elfu hamsini?
 
Ungemshauri wewe ingependaza zaidi, nimetoa maoni yangu kama nilivyo toa basiii
 
Sogea zako k.koo nunua mifuko mchanganyiko ya 45000, anza kuzunguka hasa mtaa wa narung'ombe, swahili, congo na Agrey mbona chapu tuu unarudisha hela yako mzee
 
Back
Top Bottom