Naombeni ushauri nini nisome kulingana na matokeo haya

Naombeni ushauri nini nisome kulingana na matokeo haya

brave Mwafrika

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2019
Posts
247
Reaction score
135
Mimi nilianzia QT mwaka juzi na nimemaliza Kidato cha nne mwaka Jana na matokeo yangu ni lama ifuatavyo, Civ 'C, Hist 'C, Geo 'C, Eng 'D, Kisw 'C, Phy 'C, Chem 'B, Bio 'C, Math 'A.

Umri wangu ni miaka 24

Naombeni ushauri kama nikienda chuo nikasomee nini chenye fursa?

Na Kama nikienda advance kusomea PCM au PCB, nini faida yake nikienda advance kuliganisha na chuo moja kwa moja.

Naomba ushauri wenu 🙏🙏🙏
 
Nenda chuo kama unaweza angalia vyuo kama ardhi, vya ufundi, bandari na mambo ya meli afya sijaiweka kwa sababu zangu binafsi ila unaweza kuangalia pia course mpya
 
Mkuu nakushauri achana na Mambo ya Advanced Level Nenda Chuo Kama Ada Ipo.

Nenda Chuo cha Ardhi University, DIT ,au DMI kule bandari.

Kuna kozi nyingi zinakufaa Kama kweli Una A ya Maths.
 
Mkuu nakushauri achana na Mambo ya Advanced Level Nenda Chuo Kama Ada Ipo.

Nenda Chuo cha Ardhi University, DIT ,au DMI kule bandari.

Kuna kozi nyingi zinakufaa Kama kweli Una A ya Maths.
#vipi kuhusu ajira zinapatikana kwa izo kozi??
 
#na saivi umeajiriwa wapi??
Hivi ukisoma Ardhi huwezi kujiajiri kwenye Real Estate kweli?

Hizi akili za kuajiliwa mtaziacha lini? Ardhi kubwa Tanzania bado haijapimwa kawatongozeni wakurugenzi mawilayani muingie mikataba ya kuwapimia Ardhi zao na kugawa viwanja.
 
#asante kwa ushauri wako.
 
Kasome diploma kwenye chuo cha madini course either geology, mining, mineral processing au hata hydrogeology zitakusaidia maana Kadri siku zinapozidi kwenda sector hii inafunguka zaidi
 
Nakushaur nenda kasomee unesi au hata ukunga huwez kukosa ajira watu wanaumwa kila siku na huwez mkuta nesi mtaani hana ajira kama izo kada nyengine
Naunga mkono hoja

Au kama unakipaji cha kufundisha somea ualimu wa sekondari diploma chap unaingia mzigoni
 
Kasome diploma kwenye chuo cha madini course either geology, mining, mineral processing au hata hydrogeology zitakusaidia maana Kadri siku zinapozidi kwenda sector hii inafunguka zaidi
Ni wazo zuri, lakini je asipo ajiriwa anaweza akajiajiri?

Pamoja na kwamba sector hiyo inazidi kufunguka, lakini je uhitaji wa walio somea hizo course ni mkubwa kiasi gani?

Anyway......Mimi nilimshauri kijana wangu akasomee kitu ambacho asipo ajiriwa basi hata yeye anaweza akajiajiri.

Na kwakua ufauluwake haukua mzuri sana niliamua akaanzie Veta masomo ya Mechanical Engineering kwa miaka mitatu, kisha nitamtafutia field (Mining) kama Mungu atanipa uhai ili akija kumaliza azijue kazi za mikono na iwe rahisi kuajiriwa ama hata kujiajiri.

Kabla hajaenda Veta nilimpeleka Driving course ili aanze kujiandaa pia kua professional driver wakati anaendelea kusoma Veta na leseni yake inakua.

Mwisho wa siku kijana nataka awe multiple skilled boy, na ikiwa atafanya vyema basi nitampandisha akachukue Diploma ya Mechanical Engineering.
 
Mimi nilianzia QT mwaka juzi na nimemaliza Kidato cha nne mwaka Jana na matokeo yangu ni lama ifuatavyo, Civ 'C, Hist 'C, Geo 'C, Eng 'D, Kisw 'C, Phy 'C, Chem 'B, Bio 'C, Math 'A.

Umri wangu ni miaka 24

Naombeni ushauri kama nikienda chuo nikasomee nini chenye fursa?

Na Kama nikienda advance kusomea PCM au PCB, nini faida yake nikienda advance kuliganisha na chuo moja kwa moja.

Naomba ushauri wenu 🙏🙏🙏
Yaani lugha yako Mama unapata C sawa na masomo magumu? Basi wewe inabidi tu uwe kibaka.
 
Back
Top Bottom