Naombeni ushauri nini nisome kulingana na matokeo haya

Naombeni ushauri nini nisome kulingana na matokeo haya

Mimi nilianzia QT mwaka juzi na nimemaliza Kidato cha nne mwaka Jana na matokeo yangu ni lama ifuatavyo, Civ 'C, Hist 'C, Geo 'C, Eng 'D, Kisw 'C, Phy 'C, Chem 'B, Bio 'C, Math 'A.

Umri wangu ni miaka 24

Naombeni ushauri kama nikienda chuo nikasomee nini chenye fursa?

Na Kama nikienda advance kusomea PCM au PCB, nini faida yake nikienda advance kuliganisha na chuo moja kwa moja.

Naomba ushauri wenu [emoji120][emoji120][emoji120]
Apply Biomedical engineering (DIT)kwa sasa kuna vifaa tiba vingi sana kwenye Hosp za Umma alafu wataalamu wakuvifunga na servicing wachache..
Diagnostic Radiology(Wataalam wa Mionzi ni wachache sana Room iko wazi)utapiganiwa sana hii inatolewa Muhas kwa level ya diploma.

Changamka kijana Matokeo Yako yanaruhusu

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
Soma kitu ambacho kitaa kinabamba,
Kwa ufaulu wako unaweza kusoma course yoyote ya engineering au afya.
Kasome Electrical with automation arusha tech,
Electronics and telecommunication/ Electrical and electronics St joseph,Dit, must au almaktoum college.
Ada za kuanzia certificate zikoje?
 
Mimi nilianzia QT mwaka juzi na nimemaliza Kidato cha nne mwaka Jana na matokeo yangu ni lama ifuatavyo, Civ 'C, Hist 'C, Geo 'C, Eng 'D, Kisw 'C, Phy 'C, Chem 'B, Bio 'C, Math 'A.

Umri wangu ni miaka 24

Naombeni ushauri kama nikienda chuo nikasomee nini chenye fursa?

Na Kama nikienda advance kusomea PCM au PCB, nini faida yake nikienda advance kuliganisha na chuo moja kwa moja.

Naomba ushauri wenu 🙏🙏🙏
science and laboratory dit mwanza
 
Back
Top Bottom