Naombeni Ushauri wakubwa: Nina mpango kuoa Binti wa Kimeru Dada yake Maghayo

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
17,595
Reaction score
39,893
Moja kwa moja .

Mimi ni kijana wa Kiume umri miaka 24 nipo Dar , Moja kati ya ndoto zangu kubwa katika maisha ni Kufunga ndoa kwani naamini ni katika njia kuu ya kujizuia na zinaa , kujenga heshima na kuishi maisha Bora ya kiuwanadamu na kujenga familia imara pamoja ya yote ndoa ni ibada kubwa kwetu sisi Waislamu.

Seriously , sitaki kuchelewa kuoa na kutokana na harakati za masomo nilipiga hesabu na kuweka azma kuwa nikifika umri wa miaka 25 In Shaa Allaah rasmi nioe.

Sasa katika harakati zangu bado sijafanikiwa kupata waifu material yaani chaguo sahihi la kuoa , ila baada ya kupitia Jf nikaona MaBint wa Kimeru wanasifiwa kwa uzuri na wengi wanaosema kuwa hawana makandokando mengi, basi nimeona nifanye mipango Nipige hodi kwa kina Maghayo The Mongolian Savage nivute Chombo safi kutoka Sing'isi meru..

Najua haitokuwa rahisi kutokana utata na upinzani wa Maghayo ila Mimi Hilo halitanirudisha nyuma nimeeandaa timu ifuatayo kuhakikisha yote yanaenda sawa from A to Z ;

GENTAMYCINE ; kunipigia rada za kijasusi jinsi ya kumStop Maghayo ambaye ni kikwazo na kurahisisha mipango.

Selikavu ; huyu kutoka Apha team atakuwa kama mwanasheria wangu na jopo lake kuhakikisha mambo ya kisheria yanakuwa sawa navuta jiko.

Dada yangu Shadeeya ; nampa kazi ya kufundisha Bibi harusi mtarajiwa mambo mbalimbali kuhusu Uislamu.

Nitaambatana na jopo la Wazee likiongozwa Ushimen ili itifaki zizingatiwe kwa Wazee wa kijii na Wazee wake Maghayo .

Binti wa zamani ; atakuwa kitengo cha kumfunda mwali.

Dumas the terrible , Beira Boy Intelligent businessman hawa watukwa escort team yangu Incase of any threats from Ghayos Gang in Meru or abroad to counteract it effectively.

Naombeni ushauri wana Jf kuelekea mission yangu hii na mengineyo ya kuchukua tahadhari na kufanya ili kukamilisha.

Ni ,Mimi Gun man from Joseon Adriz The Consigliere

#UziTayari
 
Unaoa mapema hivo ili upate nini au unaogopa nini?
Kuna ubaya gani kuoa mapema ? Mimi naona Faida

1. Akili inakomaa
2. Mindset inabadilika inakuwa ya kikubwa zaidi na akili inapanuka
3. Hamasa katika utafutaji inaongezeka
4. Unakuwa na watoto mapema ujanani inakuwa rahisi kuwalea na kuwaControl ukiwa na nguvu.
5. Uhakika wa kupata utulivu na liwazo ; umerudi home waifu anakupetipeti anakukiwaza na ukiwa na matamanio ni rahisi kuondoa kwa njia halali.
6. Inajenga na kuongeza uwezo wa kuongoza na kufanya maamuzi sahihi na ya busara
7. Unapata mtu wa karibu wa ndani kushaurina nae mambo muhimu.
8.Nk
 
Kufunga ndoa ni njia kuu ya kujizuia na zinaa,mkuu hivi huu ni mwaka elfu moja mia nane themanini na ngapi?
Zinaa ni kufanya tendo la ndoa na mtu ambaye sio Mme wako au Mkeo kihalali.

Sasa ukiwa haujaoa na mambo yamekuzidia ni rahisi kuzini tofauti ukiwa umesoa simple unaenda kwa Mkeo kuzidhi haja za matamanio chap , japo wahuni ambao hawatosheki hawakosekni katika kila sekta
 
Wazinifu (na mimi nikiwemo) tutakuja kusema unakimbilia nini...??

Fanya kile ambacho ni sahihi mkuu...

Ukishindwa kujuzuia na hutaki kutenda dhambi oa hii ndo njia sahihi


Tumeambiwa tuikimbie tamaa hata kwa miguu..
 
Kijana anataka waschana waliochanjwa pembeni ya macho.

Kijana anataka kufa mapema akicha mwali bado mbichi

Kijana anaonekana mjuaji Sana Kwa wanawake kumbe ni kilaza

Kijana anaangalia uzuri ndio kipaumbele chake anataka stress ya kugongewa mara Kwa mara.

Kijana endelea kujitafuta usitafute mapenzi Wala ndoa hivyo vitakuja Kwa wakati wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…