Naombeni ushauri wakuu, mke wangu amezaa na mwanaume mwingine

Naombeni ushauri wakuu, mke wangu amezaa na mwanaume mwingine

kaka habari yako pole na majukumu,nakuomba uni postie hili Jambo linanisumbua Sana naomba nipate ushauri wa watu wengi moyo wangu upone lkn naomba unifichie jina langu..

Kaka sasa liko ihvi, mimi nimeoa mwaka 2014 mpaka sasa Niko na watoto wa3 watoto wangu nawashughulikia kama Baba vizuri, lakini mwaka Jana mke wangu akabeba mimba nje ya ndoa nilikuwa safari ya miezi 3 after kurudi sikujua kama mke wangu nimjamzito maana sikumchunguza Kwa sababu nilikuwa na mwamini Sana..

Miezi ikaendelea kusogea baadae akajifungua vizuri mtoto wa kiume lakini sasa nika hesabu miezi nilie lala na mke wangu ni muda wa miezi sita, hapo ndio Nikagundua mimba sio yangu..

Nikamuuliza akakiri ameteleza anaomba nimsamee lakin nimeumia Sana mpaka sasa Bado naishi na yeye lakini Imani yangu imepotea kwake kabisa nifanyaje Kwa maana tayari amenizalia watoto 3 iyo kitu inanisumbua Hadi saa hii...
Pole mkuu
 
Kiuhalisia huyo kakosa hadhi ya mke. Mwamba anatakiwa apige chini tu kuhusu watoto una assume tu amekufa. Kwani ikitokea leo kafa watoto ndo watakosa haki ya kuishi.
Kusingizia watoto kuteseka ni kutafuta huruma ya kulea ujinga. Piga chini maisha mengine yaendelee inaumiza lakini ni bora kuliko kuendelea kumkumbatia malaya.
 
Back
Top Bottom