NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,925
Habari zenu, awali leo niliweka maana >> hii << juu ya ndugu yangu ambae ana chang moto za kusikia.
Kwa ufupi ni kwamba alizaliwa fresh ila akapata homa akiwa na miaka 9, alipigwa sindano ya kwinini kwa dozi iliyozidi matokeo yake taratibu akaanza kupoteza usikivu mpaka imekuwa ni tatizo kabisa kusikia.
Kwao naweza tu kusema pesa si haba zipo, kila siku hupewa 30 hadi 40, hivyo kwa mwezi ni kama milioni, si jambo la kushangaza kwa hali waliyonayo lakini kwa sasa naona nae kapata shauku ya kutaka kutafuta chake, anataka pesa ya kuipambania yeye .
Nipo nae karibu na hata kwenye simu huwa tunachat sana, kaniomba nimpe ushauri wa biashara ya kufungua, Yeye kanipa wazo kwamba biashara isiwe ya kuhitaji kulazimu mazungumzo sana kwa watu wengi, mimi nimepata wazo la biashara ya gym inayoendana na anachotaka ila nimeona tuunganishe mawazo tumsaidie kwa mawazo ya biashara za ziada,
Kwake mtaji wa fedha anaoweza kupewa ni milioni 20.
Mimi binafsi nimekuja kwenu wadau mnisaidie maana nae dogo naona kashafika umri flani anatamani maisha yake, mwanaume anaweza kuwa na changamoto lakini bado ana malengo yake
Miaka: 22
Jinsia: Mwanaume
Elimu: Form 4 alifaulu kwa division 2 alichaguliwa kombi ya science ila aliishia hapo kwa sababu yeye na wazazi waliona kwamba mfumo wa elimu nchi hii kwake utamshinda katika upande wa ufundihaji, jamii (walimu + wanafunzi), na pia waliona hata wenye shida hio waliofika vyuoni wanapata changamoto kupata ajira baada ya kuhitimu.