Naombeni ushauri wenu juu ya mtu mwenye matatizo ya masikio anaweza kufanya shughuli ipi ikiwa ana mtaji wa fedha ?

Naombeni ushauri wenu juu ya mtu mwenye matatizo ya masikio anaweza kufanya shughuli ipi ikiwa ana mtaji wa fedha ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Habari zenu, awali leo niliweka maana >> hii << juu ya ndugu yangu ambae ana chang moto za kusikia.

Kwa ufupi ni kwamba alizaliwa fresh ila akapata homa akiwa na miaka 9, alipigwa sindano ya kwinini kwa dozi iliyozidi matokeo yake taratibu akaanza kupoteza usikivu mpaka imekuwa ni tatizo kabisa kusikia.

Kwao naweza tu kusema pesa si haba zipo, kila siku hupewa 30 hadi 40, hivyo kwa mwezi ni kama milioni, si jambo la kushangaza kwa hali waliyonayo lakini kwa sasa naona nae kapata shauku ya kutaka kutafuta chake, anataka pesa ya kuipambania yeye .

Nipo nae karibu na hata kwenye simu huwa tunachat sana, kaniomba nimpe ushauri wa biashara ya kufungua, Yeye kanipa wazo kwamba biashara isiwe ya kuhitaji kulazimu mazungumzo sana kwa watu wengi, mimi nimepata wazo la biashara ya gym inayoendana na anachotaka ila nimeona tuunganishe mawazo tumsaidie kwa mawazo ya biashara za ziada,

Kwake mtaji wa fedha anaoweza kupewa ni milioni 20.

Mimi binafsi nimekuja kwenu wadau mnisaidie maana nae dogo naona kashafika umri flani anatamani maisha yake, mwanaume anaweza kuwa na changamoto lakini bado ana malengo yake

Miaka: 22

Jinsia: Mwanaume

Elimu: Form 4 alifaulu kwa division 2 alichaguliwa kombi ya science ila aliishia hapo kwa sababu yeye na wazazi waliona kwamba mfumo wa elimu nchi hii kwake utamshinda katika upande wa ufundihaji, jamii (walimu + wanafunzi), na pia waliona hata wenye shida hio waliofika vyuoni wanapata changamoto kupata ajira baada ya kuhitimu.
 
Habari zenu, awali leo niliweka maana >> hii << juu ya ndugu yangu ambae ana chang moto za kusikia.

Kwa ufupi ni kwamba alizaliwa fresh ila akapata homa akiwa na miaka 9, alipigwa sindano ya kwinini kwa dozi iliyozidi matokeo yake taratibu akaanza kupoteza usikivu mpaka imekuwa ni tatizo kabisa kusikia.

Kwao naweza tu kusema pesa si haba zipo, kila siku hupewa 30 hadi 40, hivyo kwa mwezi ni kama milioni, si jambo la kushangaza kwa hali waliyonayo lakini kwa sasa naona nae kapata shauku ya kutaka kutafuta chake, anataka pesa ya kuipambania yeye .

Nipo nae karibu na hata kwenye simu huwa tunachat sana, kaniomba nimpe ushauri wa biashara ya kufungua.

Kwake mtaji wa fedha anaoweza kupewa ni milioni 20.

Mimi binafsi nimekuja kwenu wadau mnisaidie maana nae dogo naona kashafika umri flani anatamani maisha yake, mwanaume anaweza kuwa na changamoto lakini bado ana malengo yake

Mkuu; Awali ya yote pole kwa mapito anayopitia huyo ndugu yako.
Tukirudi kwenye hoja yako labda utusaidie kwa kutoa maelezo kidogo kadri uwezavyo:

1. Ndugu yako ana kiwango gani cha Elimu,

2. Ukiacha masikio, je kuna viungo vingine vina matatizo?

3. Ndg.yako ameshajaribu shughuli / kazi gani na akaona anakwama wapi?

Maswali yaliyoulizwa ni kwa lengo la kumtanabahisha ndg. yako kwamba kuwa na kiungo kimoja chenye hitilafu hakumzuii yeye kutumia vile viungo vilivyo vizima. Kwa macho anaona, kwa mikono ataweza kufanya shughuli nyingi tu, kwa miguu atakwenda na kurudi, n.k.n.k.

Kama ana taaluma yoyote au anaweza kusoma na kuandika anao uwezo wa kufanya biashara(Ujasiriamali) e.g. Kuanzisha na kuendesha mgahawa, kujenga nyumba za kupanga au G/houses, kununua na kuuza nguo, kuendesha Hardwares n.k. zote hizo kama ikitokea mazungumzo yeye atatumia njia ya kuandika wakati wa kutoa hoja na majibu au anaweza kuajiri mtu akawa chini ya uongozi wake.

Anaweza kuwa mfugaji kibiashara wa wanyama wadogo-wadogo na kuwauza.

Aidha Fursa hutegemea na eneo mtu alipo. e.g. Fursa zilizo Dar sio sawa na Fursa zilizo huku Umasaini.
 
Umri: miaka 22

Elimu: Alimaliza form 4 divisoni 2 ila hakuweza kuendelea,

changamito ya viungo ni masikio tu

SIjawahi kuona anafanya shughuli nyingine, ndio anataka kuanza nasmi (better late than never)
 
Hivi Dawa za Quinine nani kwa nini ziliruhusiwa kutumika pamoja na madhara yake makubwa...

Asilimia 90 ya viziwi waliozaliwa wazima, ukiziwi wao umetokana na side effect za madawa hayo.
Acha tu yani, huyu dogo bila hili tatizo nlikua namuona mbali, form 4 tu alipoishia alipata division 2 licha ya changamoto zake,
 
Kwa nini hakuendelea na shule?
Mazingira ya shule na vyuo vya Tanzania ni kazi sana kwa mtu mwenye hizo changamoto kusoma.

Si shule tu bali hata jamii kwa ujumla kuanzia walimu na wanafunzi

hata wanaohitimu vyuo wamejikuta kwenye dilemna ya kubaguliwa wazi wazi kwenye soko la ajira badala ya kupewa vipaumbele, kwenye fomu wanapamba kuonekana wanajali lakini uhalisia ni tofauti
 
Vipi dogo ana mpenzi/mchumba?
Yaani anachakata Mbususu? Kama bado mwambie aanze mara moja wakati mwingine kuchakata Mbususu husaidia kufungua akili katika utafutaji.
Mpe pole sana lakini bado ana nafasi ya kufikia malengo yake asikate tamaa.
 
Mazingira ya shule na vyuo vya Tanzania ni kazi sana kwa mtu mwenye hizo changamoto kusoma.

Hata jamii kwa ujumla kuanzia walimu na wanafunzi

aliweza kwenda form 5 ila aliacha
Inawezekana kabisa kusoma, labda tu aliamua tu kuacha.

Nimesoma Udom Kuna viziwi watatu na wasioona watatu ninaowafahamu tuligraduate nao.
 
Umri: miaka 22

Elimu: Alimaliza form 4 divisoni 2 ila hakuweza kuendelea,

changamiti ya viungo ni masikio tu

SIjawahi kuona anafanya shughuli nyingine, ndio anataka kuanza nasmi (better late than never)
Mkuu, Huyo kijana anauwezo kuzidi hata mwenye masikio mazima.
Kwa maelezo yako na kiwango chake cha elimu ukijumlisha na uwezo kifedha, hebu mshauri aanzishe biashara iliyotulia mahali i.e. isiwe ni biashara ya kukimbizana - kimbizana au kusafiri sana. Mfano wa biashara iliyotulia ni kama vile Hardware, nyumba za kupangisha au fremu, Stationeries, maduka ya bidhaa ndogo-ndogo, Tenda za kutoa huduma ya vyakula e.g. boarding schools n,k,
 
Afungue ofisi,afanye biashara za real estate,aanze mdogodogo,kununua na kuuza,kwenye ofisi atafute msaidizi,kwa hiyo ataitajika Sana kuonana na wateja face to face ,mfanyakazi wake atahusika,au awe wakala wa bima,za magari n.k
 
Inawezekana kabisa kusoma, labda tu aliamua tu kuacha.

Nimesoma Udom Kuna viziwi watatu na wasioona watatu ninaowafahamu tuligraduate nao.
Kwa upande moja nakubaliana na wewe ila kwa upande mwengine kwa mazingira ya hapa Tanzania naona dogo alijipunuzia mzigo.

Kusoma ni jambo moja, ila kuja kuajiriwa ni kitu kingine, hawa watu makundi maalum ilibidi wawe vipaumbele lakini kwa nchi kama yetu mambo ni mazito

Mkuu nami niliwahi fatilia wapo wenye changamoto hizo wanaofika vyuoni lakini kwenye suala la ajira nimeona wanapata changamoto mno.

hata interview hazijawazingatia, hukuti mtu wa lugh za alama, kuna mdau aliwahi funguka humu ana degree ya statistics. hata huko vyuoni hakuna watu wa lugha za alama, hii inafanya elimu kuwa ngumu sana na wenye changamoto kutumia bidii mara 3 zaidi ya wale wengine

Kuna Member humu alikua na Tatizo kama lake pitia uzi wake, Dhihaka na Kejeli zinaumiza Sana >> uzi huu hapa <<
 
Kuna vitu hujaviweka sawa Ndugu Mtoa mada

Kuna tofauti kubwa kati ya DEAF PEOPLE na HEARINGS IMPAIRED PEOPLE,..Kuna vile vyama kwa ajili ya DEAF PEOPLE mfano CHAVITA..na HEARING IMPAIRED ambao wanapata shida kwa kuwa inawalazimu kusoma na wanaosikia.

Anyway..Kama muhusika amesoma japo ngazi ya Degree basi anaweza akafungua just a Small Private Company katika Sector zitiatazo kisha akawa Director.. then akaunda Board of Directors within that board anamuajiri msimamizi mwenye matatizo aina yake ambae anamuamini na aliemsomi mwenye uwezo na ujuzi wa kutosha.

Na yeye akawa hapo kuweza kumonitor each action’s and responsibilities..Miongoni mwa izo Small Companies inaweza ikawa mojawapo kati ya hizi:-

  • Art, design and photography company
  • Copywriting, writing and editing company
  • Interpreter
  • Information technology and engineering
  • Finance and business administration company
  • Teacher for students with Special Needs
  • Professional Sign Language Interpreter and Translator.
Kingine aangalie yeye mwenyewe ana ujuzi gani na afanye hicho hicho, au anapenda fani ipi apate mafunzo afanye..Kazi zipo nyingi kama vile ushonaji (afungue kampuni ndogo ya ushonaji au afungue garage).

Ajaribu kuangalia mazingira yaliyo mzunguka na aangalie ni kitu gani unaweza kujishughulisha nacho..kikampa faida cha msingi aangalie kitu gani anakipenda ajifunze afanye..hamna kinachoshindikana..ni moyo wake tu wa uvumilivu na uaminifu ndo ufunguo wa mafanikio.

Kwa kumalizia anaweza kujiunga na vyama vyao vya watu wasiosikia wana network yao kule atapata exposure, utajuana na watu..hawezi jua MWENYEZI MUNGU kampangia nn mbeleni..yaweza kua huko ndo kuna rizki yake.

Dua zangu nyingi kwako/kwake kila la kheri🙏🙏🙏
 
mpe pole sana, anaweza akafanya biashara yoyote ile kwasababu anaona anatembea na vitu vingine vyote anaweza kufanya, kwa hiyo 20m anaweza akafungua Microcredit,
 
Inawezekana kabisa kusoma, labda tu aliamua tu kuacha.

Nimesoma Udom Kuna viziwi watatu na wasioona watatu ninaowafahamu tuligraduate nao.
Bullying mzee ndo tatizo kuna dogo alipata hili tatizo nae alipata akiwa advance ila bullying ilimtoa kweny reli alifaulu ila mzee wake anasema kuna kipind alikuwa anarudi hata wiki akija kwao anasema anataniwa na hataki kurudi shule basi ..Basi mzee wake anambembeleza anarudi mpaka akamaliza ila ajira alikosa ila alisoma mpaka chuo.
 
Kuna Member humu alikua anaitwa MPAUKO (RIP) alikua na Tatizo km Hilo la kusikia Anadai alisoma kwa Shida Sana Chuo kuanzia Lecture had wanafunzi wenzake Walikua Wanamcheka na Kumdharau Miufupi Unaweza kuona inawezekana kusoma ukiwa na Matatizo haya ila Dhihaka na Kejeli zinaumiza Sana
 
Uzi wake >> huu hapa <<

Aendelee kupumzika kwa amani
 
Back
Top Bottom