Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Naona aibu kuuza maji barabarani nisaidieni

Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips [emoji489] na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.

Huu sio mwandiko wa yudizimu.
 
Kwahiyo elimu yake inamsaidia kuuza maji barabarani?

We kweli mwehu?
mimi na wewe nani mwehu,wewe unamwambia asiuze maji,mimi na mwambia uza,sasa elimu inamsaidia nini hapo?namshukuru mungu sijasoma ila nimefanikiwa kuliko walioenda shule na nimewaajiri kibao tu waliosoma
 
Habari zenu jamani mimi ni kijana mdogo mwenye umri wa miaka 26 nimemaliza chuo cha Dar es salaam mwaka jana. See saizi nipo apa Dar es salaam Tandika nakaa na kaka angu ndoananipiga jeki nakaa kwake akienda kazini na mke wake wananiachia buku tu la msosi usiku wakirudi shemeji anapika msosi tunaufinya.

Changamoto ilianza majuzi huyu shemeji Ana roho mbaya kweli kumbe kipindi chote kaka angu huwa anampa 2000 ili anipe pesa ya msosi afu yeye anakata ananipa buku, nilikuja kugundua juzi broo aliposema kwa sauti nanukuu.,(hiyo buku mbili utampa dogo ya msosi) nikasema afadhari nitanunua namm Leo chips [emoji489] na Pepsi nijimwayemwaye, Sasa chaajabu shemeji akaja kunipa buku tu hapo tukaanza kugombana sasa akaanza kunifyezuri na kunifedheshesha mbele ya majirani wa kizaramo wavaa vijora, akisema tena kwa sauti ati amenichoka najaza kitambi tu kazi Sina nabweteka Kati pesa nizakaka angu.

Jana ilibidi yote nimwambie broo huku nikiwa na hasira sana kuliko mwanaume aliyemfumania mkewe . Broo akaniambia yote yaishe atanipa mtaji wa kazi.

SASA chaajabu Leo asubuhi naona ameniletea maji ya uhai kama Dazani tano hivi na MO energy kama dazani saba eti anasema nisimame kwenye mataa ya Sudani Temeke nianze kuuza huku nimebeba mimaji kichwani amesahau kuwa mimi nina degee kutoka UDSM chaajabu hajaniachia hata sent mpaka mdaa huu sielewi nakula nini wenyewe wameenda kazini, naombeni ushauri nifanyeje.

Funga macho fanya kuuza hayo maji maana huna kingine cha kufanya. Ila unaweza ukuza huo mtaji kaka yako aliokupa, ukawa unauza maji mengi zaidi. Baadae unatafuta kijana anakuwa anakuuzia.
 
Funga macho fanya kuuza hayo maji maana huna kingine cha kufanya. Ila unaweza ukuza huo mtaji kaka yako aliokupa, ukawa unauza maji mengi zaidi. Baadae unatafuta kijana anakuwa anakuuzia.
Duh
 
"Some times we need to put academic qualifications aside and husle like a school drop out because your degree doesn't pay bills"

Mkuu hata Mimi ni graduate lakini sichagui kazi nishapiga saidia fundi,kuuza duka kwa kujitolea mshahara hamna ni msosi tu.Sasa mkuu kwenye utafutaji wa pesa hakuna aibu utaendelea kuomba mpaka lini mzee.

Labda nikushauri nenda mkoa ambao hufahamiki then piga kazi... kumbuka "Mwanaume akiwa na pesa ni sawa sawa na demu kuwa mzuri".

Pia last but not least ukipata mtaji usisahau kubeti kwa akili nyingi ndo njia ngumu na rahisi kutoboa kwa graduates...
Hhhhhhaaaa eti kub3t
 
Sikiliza kijana. Nenda kafanye kazi. Hujaandikwa chapa usoni. Tena yakiisha ingia hapo afiya chukua mengine. Pia kama hapo home iko friji funga kandoro peleka shule ya msingi au stendi hapo tandika unaweza ingiza zaidi ya 10,000 kwa siku. Ukitoa elfu mbili ya umeme kwa siku na elfu moja ya vifuko. Na buko ya chakula Elfu saba faida kwa siku.
Sasa 7000 kwa siku halafu future yako itatimia lini
 
mtu ana miaka 26 halafu kasoma, shule ya msingi, secondary (o-level na aA-level) na degree halafu anajiita yeye ni mtoto mdogo. kweli mambo ni mengi, muda mchache
 
Very sad indeed. Hii inaweza kuwa stori ya kutunga lakini ina ujumbe mzito sana.

Mhitimu wa chuo kikuu anauza maji barabarani, jambo la ajabu sana.

Na wengine wanakudhihaki humu na kushangilia kwamba wacha likome na madigrii yake!

Tumekuwa na jamii ya ajabu sana ambayo inaona ni jambo la kawaida muhitimu wa chuo kikuu kuwa muuza makopo!?
Kumbe n bora aishi na digrii yake kwa shemej yake??.

Soma alama za nyakati.
 
Yani hii nchi ngumu sana kiongozi halafu saizi ukiwa msomi huna kazi wala pesa mitaani wanakudhihaki
Sio nchi ngumu, na sio kudhihakiwa.

Jamii inategemea kuona ww na usomi wako unakuwa mfano wa kuigwa na wengine..... Msomi n mtu anayeaminiwa sana na jamii coz wanaamini ana uwezo wa kufikiri nje ya box.
Inaleta picha gan msomi huyohuyo yupo directionless. Komaa na mawazo ya Kivumishi Kielezi . ilee hio digrii nyumban ukifika mda wake itazaa mapacha.
 
Kakako na shemeji yako wana akili sana. Kama utashindwa kujifunza kutoka kwao itakuwa ngumu sana mtu mwingine akufundishe na ukaelewa.
 
Sawa,Huwezi hadharani, kwa siri je? unaweza?, yaani usijulikane unauza maji wateja waje wanunue kisiri siri.
 
Back
Top Bottom