Uchaguzi 2020 Naona CHADEMA inavyokwenda kuishangaza Dunia

Dawa ya moyo ulioumia na hauna matumiani dawa yake si kujifariji tu, Bali ni kuukubali ukweli kwamba hicho kinachouumiza moyo hakiwezekani Bora ukatafuta namna nyingine ya kuutuliza moyo Kwa maumivu hayo

Mpaka hapo, Chadema hamjaanza kutafuta dawa ya maumivu yenu

Jiambieni ukweli ili mpate nafuu ya maumivu
 
Kwa maajabu gani iliyofanya zaidi ya kuinanga serikali iliyoko madarakani. Kwa upande wangu naiona chadema ikipoteza majimbo yote tegemezi.

Huu ni mwaka naona chadema ikipoteza nafasi ya kambi upinzani bungeni.
 
Mateka ni wewe
Maandiko matakatifu (Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu) yanaakisi fikra zako kama walivyonena wahenge Fuumbo mfumbie mjinga, mwerevu atang'amua. Yaani, wewe na wenzako mnao shabikia uovu, uhuni na uwongo wa viongozi wa CHADEMA ni kama Bendera kufuata upepo.

Chama kimevurugwa na kinaendelea kuvurugwa na viongozi wenyewe, kama wanavyokiri wabunge wanaokihama. Katika hali hiyo, chama kinahitaji miujiza kukubalika na jamii. HUO NDIO UKWELI MTUPU unapaswa kumezwa na wahusika japo mchungu, .
 
Hizi ishu mbili kwa CCM ni Kama ile kitu wanasema ukisimama nchale ukikimbia nchale yani either way ya option haitawasaidia maana wakitangaza Leo kuongeza watumishi mishahara itatafsirika ni rushwa wasipoongeza pia mbaya maadam washaamua kuwalia watumishi mavi waendelee kula mavi kila mtu ajue lake .......
 

Watapandishia hiyo mishahara ufipa au?
Kama pesa kidogo walizokuwa wanapewa wameshindwa kuwapa hata viongozi wa mikoa iatakuwa kutatua matatizo ya nchi?
Pesa yote ya ruzuku pamoja na michango ya wabunge na wahisani, bado hata banda la kupumzikia hawana wataweza kuhudumia taifa?
Chadema waseme ni wafanyakazi wangapi ngazi za mikoa wanalipwa na chama kama posho au mishahara?
Tusitaniane bwashee.
 
Yapo mengi sana, huyu bwana kaua biashara nyingi sana za watu sababu ya kukurupa na kujifanya kagundua wezi wakati yalikuwa ni mapungufu ya serikali ya ccm yenyewe ambayo alitakiwa kuyashughurikia kwa umakini, na kwa kushirikisha wafanyabiashara.

kwa mfano,kwa kupitia TRA wafanyabishara wengi sana wamefirisika na kufunga biashara, kwa sababu za tu kwa mfano hawakuwa na efd mashines, au hawajalipa kodi muda mrefu, lakini mwisho wa siku baada ya biashara nyingi kuwa zimefungwa na kukosesha wananchi ajira, akaja na kasheria ka msamaa wa faini za machelewesho ya kodi, ikiwapo na kuwapa fursa wafanyabisha kuanza kulipa malimbikizo ya kodi kwa muda unaowapa nafuu. by this time tayari aliishaua biashara nyingi sana, hawa hawahitaji CHADEMA awaambie hawa wanamsubiri wamunyooshe.
 
Kuina
Kwa maajabu gani iliyofanya zaidi ya kuinanga serikali iliyoko madarakani. Kwa upande wangu naiona chadema ikipoteza majimbo yote tegemezi.

Huu ni mwaka naona chadema ikipoteza nafasi ya kambi upinzani bungeni.
Kuinanga serikali iliyoko madarakani ni jukumu halali la upinzani waisifie iweje? Halafu wajinga wachache Kama nyie ndio mawazo yenu yanarudisha nyuma maendeleo. Swala la sekondari bure ilikuwa ni agenda ya chadema tunapokuwa na strong opposition ndio wananchi wanafaidika kwasababu chama tawala kinaogopa kikivurunda kinatolewa Sasa nyie mlivyo wajinga mnaombea upinzani ufe aiseee akili ndogo ni tatizo unatakiwa ujue The stronger the opposition the more people benefit and vise versa.Kuturudisha kwenye chama kimoja nikurudisha nyuma maendeleo.
 
Kila kundi lililoharibiwa maisha linasubiri kulipa kisasi chake na vitakuwa ni visasi vya haki.
 
Kuna jamaa mmoja ni muuguzi anasema alikopa nmb akafanyia maendeleo akakopa crdb halkadhalika na 1/3 yake ikabaki ilipokuja bodi ya mikopo isiyozingatia 1/3 Sasa anapata 60,000/= elfu stini Tena mikopo yote mipyaaaaa niambie mtu Kama huyu anaanzaje kuopenda CCM.
 
Chadema ni vyema ingefanya siasa safi ikiwa ni pamoja na kupongeza baadhi ya juhudi ambazo serikali inazifanya. Sio kila kitu ni cha kusema vibaya jamani. lol
 
Chadema ni vyema ingefanya siasa safi ikiwa ni pamoja na kupongeza baadhi ya juhudi ambazo serikali inazifanya. Sio kila kitu ni cha kusema vibaya jamani. lol
Hi sio lazima mbona CCM mko obsessed Sana na masifa ? No wonder jp mmempa sifa za uungu TBC
 
Hi sio lazima mbona CCM mko obsessed Sana na masifa ? No wonder jp mmempa sifa za uungu TBC
Uungu mtu wapi wakati mambo anayofanya yanaonekana kwenye mazuri si vibaya kupongeza mpendwa. Na pale anapokosea ruksa kusahihisha kwa kutokutumia lugha ya kejeli.
 
Hata wanajeshi hawana combat. Navy white siku hizi zinashonwa kariakoor na hela ya Askari, boot hakuna
 
Unajua hata mgonjwa anaekaribia kufa kule mwisho mwisho huwa anakuwa amechangamka hadi anatia matumaini kwa wauguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…