Naona ipo siku nitaiacha hii kazi ya ualimu ni wakati Sasa wa Kutengeneza mifumo

Inakuwaje umeingia mkataba na CWT
 
Afisa utumishi sio cheo Cha mwisho ANDIKA barua ya kuachana na CWT na kujiunga na hicho chama kipya ukiwa umeambatanisha na form za chama
kipya harafu uone kama afisa utumishi atapinga, akikataa akujibu Kwa barua
Nimeshaandika barua ya kusitisha makato ya CWT na nakala za fomu za kujitoa uanachama Nilizifikisha ofsini kwao, njia zoote za kujitoa CWT nimezipitia, nimeandika barua tena Kwa mara ya pili Kupitia kwa mkurugenzi kuomba kusitishiwa makato, hiyo ndio kete yangu ya Mwisho ya uungwana asipoifanyia kazi nitamuona kwamba ni mkaidi. Maana kawazuia Ma-afsa utumishi wengine wasiondoe mtu wa CWT ukiwafata hao afsa utumishi wenyewe wanakwambia nimfate mkuu wa idara, ukimfata mkuu wao wa idara anakwambia uende CWT, ukienda CWT wanakurudisha kwa afsa utumishi.
 
Yaja halmashauri unayofanyia Kazi, tumchane huyo afisa utumishi
 
Upo halmashauri ipi, taja tu usiogope, tumpelekee moto
 
Acha kumpa mwenzako mawazo ya kimasikini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…