Naona ipo siku nitaiacha hii kazi ya ualimu ni wakati Sasa wa Kutengeneza mifumo

Pole sana Mwalimu.
Umelaumu sana uongozi wako lakini inaelekea hujui namna ya kujitoa kwenye chama chako. Epuka sana lawama. Ungeeleweka sana kama ungeomba kujua utaratibu wa namna ya kujitoa kwenye chama cha wafanyakazi mf. CWT.
Walimu msijishushe sana hadi mkaeleweka vibaya. Tunawategemea sana sanaaa, nyinyi ni watu muhimu sana katika jamii

Ukitaka kujitoa fanya hivi:
Andika notisi ya siku 30 kwa DED ukimtaarifu kuwa unatarajia kujitoa CWT; nakala peleka kwa Katibu CWT wilayani kwako.
Baada ya siku 30 makato ya 2% yatasitishwa.
Then ukitaka kujiunga na chama kingine utajaza fomu maalum baada ya kuelimishwa. Ukiridhika nao mwandikie DED wako ukimtaarifu kuwa akate kiasi fulani kwenye mshahara wako kwenda chama kipya. Ambatisha hiyo fomu.
Fanya hivyo Mwalimu,ni haki yako.
Lakini ni vizuri chama ndicho nikufuate kukubembeleza.
Sorry, huu si uzi mpya. Namtetea mwalimu wetu.
 
Asante.

Nilifanya hivyo mwaka Huu mwezi wa pili, niliandika barua ya kumtaarifu DED kujiondoa uanachama wa CWT nakala nyingine nikapeleka kwa karibu CWT wilaya (copy zote ninazo), Nikaandika barua nyingine ya kujiunga na chakuhawata ambapo wamenikata kwa muda Sasa, Lakini Cha kushangaza mwezi uliopita nikaona makato ya CWT (chama ambacho nilishajiondoa kabla)..kitendo Cha kwenda kufatilia na kuuliza kwanini nimekatwa chama ambacho nilishajiondoa na fomu nilimuachia katibu wa CWT? Ndio naona danadana zikipigwa, mkuu wa idara utumishi ananiambia niende CWT waniandikie kwamba nimeshajitoa, CWT wanasema wenyewe hawawezi kuniandikia nirudi utumishi ndio wenye uwezo wa kunitoa.
 
Wewe kama unataka kuacha ualimu ni vizuri uache, sasa hapa unampigia kelele nani? Ulivyoandika humu ni pumba na ujinga mtupu! Kama hutaki kazi ya ualimu ondoka haraka sana kwani nani alikuingiza kwenye kazi hiyo!
 
Muone Afisautunishi wa walimu,Katibu wa TSC wilaya yako.
Mueleze kila kitu,yataisha.
 
Jaribu kutumia mamalaka nyingine pia kupata haki yako. Unaweza kwenda hata kwa viongozi wa kisiasa kama Mkuu wa Wilaya na mbunge wa eneo husika, naamini watakusaidia kutatua changamoto unayoipitia
Hakuna wa kukusaidia kwenye hii Dunia isipokuwa ni wewe mwenyewe, aache kazi akapambane kitaa atatoboa tu. Kazi ya ualimu ya kisenge sana
 
Nyie ndo walimu waoga waoga, ukienda jinga jinga lina miaka Sita linasubiri kuajiriwa hilo ni jalimu pumbavu lisilojitambua. Walimu wote wana kasoro kubwa sana kwenye ubongo
 
Unarudi shuleni na mawazo. Nafundisha physics na Mathematics form one mpaka form four, nitapata morale ya kufanya kazi? Itoke wapi? Mimi ni mtaaluma majukumu ya kitaaluma nitayatimizaje huku nikiwa na mawazo?
Pole sana, Ndugu. Weka mipango na mikakati, utafanikiwa nje ya ajira ya Ualimu.
-
Nimepita huko, nafahamu na naelewa unachopitia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…