Naona jamii yetu ya siku hizi wanaona single parenting kama kitu cha kawaida

Naona jamii yetu ya siku hizi wanaona single parenting kama kitu cha kawaida

Almost wote huge percentage!! rate ya divorce ya miaka ya 1970 kurudi nyuma huwezi kulinganisha hata kidogo na divorce rate ya miaka ya 1990 na kuendelea. Miaka ya 1970 kurudi nyuma ndoa kuvunjika ni chache sana, mimi babu na bibi zangu wooote mzaa baba na mama na wadogo na kaka zao na majirani zao hakuna walioachana ila kizazi chetu macousins wengi wameachana, kizazi cha watoto wetu ndiyo balaah ndoa haifiki 5 years.
una uhakika ni babu na bibi wote??
 
Wazazi hamkuwajibika ipasavyo
Mtoto umleavyo ndyo akuavyo
Unakuta familia watoto wa kike sita wote wamezalia nyumbani na mzee anakenua tu Meno
 
Sijui kwa upande wenu ila kila nikitizama siku hizi single parenting imekuwa kama trend yaani kitu fulani ambacho vijana hawakiogopi.

Nikitizama zaidi nawaona hawa wana saikolojia/motivation speakers ambao kidogo wamebase kwenye biashara hili jambo wamelichukua kibiashara zaidi. Mfano siku hizi kuna makongamano ya jinsi ya single father/mother wanavyo takiwa waleee watoto, nimeona imekuwa kibiashara zaidi.Naona kuna vipindi mpaka vya TV vya kuwaelimisha single parenting jinsi ya kuwalea watoto wao.

Ila sijaona juhudi za kukazania jinsi ya kuwajenga vijana wapende maisha ya familia, maisha ya ndoa, umuhimu wa familia.

Najua jamii yetu imekengeuka vijana siku hizi hawataki kubeba majukumu yao, jamii yetu imekuwa shaghala baghala,Jando na unyago hatutaki kuvisikia na maisha ya wakubwa ambayo vijana wanatakiwa kujifunzo kupitia wao nao wanahisi maisha ya hovyo.

Kila nikitizama kama tumeamua kuupromote huu usingle parenting now kupitia media na hizi semina (sio kitu kibaya kuwatia moyo single parents) ila naona kama mafunzo ya kuwaeleimisha vijana kuishi maisha ya ndoa na familia yao kama tuna yapuuzia.

Sijui kwa wengine ila kwangu kuna kitu na kiona sio kizuri kwa jamii yetu ijayo.

Naamini familia bora,hutengeneza jamii bora na taifa bora.
Hongera angalau Kwa kuligusia hili, baadhi ya wachangiaji naona nao kama ni walewale!🤔🤔, Anyway,... Nakazimika kukubaliana na nadhari ya Darwin, (EVOLUTION) kwamba the society is passing a critical ethical and cultural evolution!
Taasisi ya ndoa SASA haionekani kama ni kitu Cha kukitetea na kukipigania Kwa mustakabali wa jamii na taifa lenye afya.
Saikolojia inaeleza wazi, mtoto aliyelelewa na mzazi mmoja hawezi kuhandle familia, inayokabili mikiki na changamoto lukuki.
 
Siku hizi kila kijana anakwambia atazaa mtoto anampeleka kwa bibi na babu yake.
 
Shetani ndo anata iwe hivyo japo huo haukuwa mpango wa Mungu
 
Back
Top Bottom