Naona kama kuna upepo wa wanaume kuacha kutongoza wanawake unakuja taratibu

Demu akivaa hivyo maana yake yupo mawindoni ukimwita tu inakutoka ten fasta chips + mishikaki na soda bado nauli boda kurudi kwake
 
Huu uzi kiboko, saa nzima imepita lakini sijaona mchango wa mwanamke hata mmoja. Wanaandika halafu wanafuta, wanaandika tena halafu wanafuta..
Sasa hapo tutacomment nini kwa mfano?
Wanaume wamechagua style ya maisha yao na wameona kuwa ni sawa kuishi hivyo.
Zama za leo wanaume wengi wanashindana na wanawake, wanasuka nywele, wanavaa hereni, wanafanya makeup, utakuta mwanaume ananukia marashi ya kike!
Ukichanganya na nyimbo zao za sasa za kulalamika, hizo nguvu za kutongoza watazitoa wapi?
 
Binafsi Mwanamke anaepaka makeup au yale manywele marefu wengine unakuta yana rangirangi kwakweli hawajawahi kunivutia naona ni kama pambo fulani tu lililopendeza ila halina faida kama mdoli.

Hata hapa mtaani kwetu sijui nani kamdanganya Hidaya zamani alinivutia sana kwa ngozi yake ya asili, nilikutana nae dukan akiwa kasuka nywele zake kwa staili flan ya mistari kurudi nyuma kwakweli alikua hachoshi kumuangalia.

Sahivi anakula makeup hadi nikikutana Nae nimemsahau na makucha yale ya kubandika kama shetani anatafuta ukoo
 
Dada! Hiyo sampuli uliyoitaja haiko kwenye kundi la wanaume mnaoingia gharama za kujiremba ili tuwaombe namba na kuwatongoza! Wanaume wanaojitambua hata wewe unawafahamu! Wanaume wanaojitambua hawataki mwanamke mwenye makeup, aliyetoboa sikio zaidi ya mara moja, aliyetoboa pua, ulimi, tattoo, matako bandia, mwongeaji saana, n.k.! Zaidi ya yote anayeomba hela kichefuchefu! Tumewashtukia
 
Tunatafuta pesa mzee, ukitongoza leo kesho unaambiwa shida zote; gas imeisha, kodi imeisha, sijui mama anaumwa, birthday, nywele zimefumuka nk ukipiga hesabu inasoma 1.5m ndani ya saa 24 je kwa mwezi utatoboka kiasi gani?

Acha tutafute pesa kwanza
 

Geez!

Sounds like you're blaming men for predicaments in your life. Are you married or still single ? You spew bile and bitterness.
 
Wanasemaga real recognize real hii haipingiki.
Na ndio maana hata tukowasifia kinafiki wanakuwa unconfortable kwasabbu wanajua mkikutana man to man .

Picha ya studio
Ikapigwa msasa kweny photoshop
Retouch za kutosha sijui frequency separation
Utakuta other brothers wanai
Sifia pisi pisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…