Naona kuna kelele na nguvu nyingi sana huku mitandaoni kuhusu uchaguzi wa TLS hebu mnielimishe ina uzito gani hasa!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Kumradhi wanabodi kuuliza si ujinga naona tu nguvu nyingi sana zina tumika kuhakikisha TLS Inapata kiongozi fulani. Pengine tofauti na jumuiya zingine nyingi ambazo wahusika huchaguana tu na sa nyingine huchaguana kimyakimya lakini kwa TLS hali ni tofauti sana

Natamani sana kujua nini nguvu ya TLS kwa kiwango cha kuifanya uchaguzi wake uvutie watanzania kwa wingi namna hii!!
 
Tanganyika Law Society (TLS) ni chama/jumuiya ya Wanasheria wa Tanganyika (Tanzania Bara). Wanachama wake ni Mawakili wa Serikali (Public) na pia wa kujitegema (Private). Na imeundwa kisheria kwa sheria ya BUNGE. Kwa hiyo kwa namna yoyote huwezi kuitenga TLS na serikali, japokuwa ni taasisi huru. Miswada yote inayopelekwa na serikali Bungeni, hupita pia TLS kwa ajili ya ushauri. Hata hivyo miaka ya karibuni inadhaniwa TLS kuingiliwa na siasa za vyama au harakati; mambo ambayo yanaweza kuzua hofu kwa watawala. Kwa hiyo ni wazi uchaguzi wa Rais wa TLS huangaliwa kwa jicho la tatu...!
 
Hamna kitu, mwabukusi ni sawa na simba aliyetengenezwa kwa tofali za barafu, jua likiwaka anayeyuka
 
Kumradhi wanabodi kuuliza si ujinga naona tu nguvu nyingi sana zina tumika kuhakikisha TLS Inapata kiongozi fulani. Pengine tofauti na jumuiya zingine nyingi ambazo wahusika huchaguana tu na sa nyingine huchaguana kimyakimya lakini kwa TLS hali ni tofauti sana

Natamani sana kujua nini nguvu ya TLS kwa kiwango cha kuifanya uchaguzi wake uvutie watanzania kwa wingi namna hii!!
TLS ni chama cha mawakili na nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria, unategemea CWT itayumbisha nchi? pia ili uwe mwanachama wa TLS lazima uwe na degree + uwe wakili tofauti na CWT, CCM n.k
 
Back
Top Bottom