The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Tanganyika Law Society (TLS) ni chama/jumuiya ya Wanasheria wa Tanganyika (Tanzania Bara). Wanachama wake ni Mawakili wa Serikali (Public) na pia wa kujitegema (Private). Na imeundwa kisheria kwa sheria ya BUNGE. Kwa hiyo kwa namna yoyote huwezi kuitenga TLS na serikali, japokuwa ni taasisi huru. Miswada yote inayopelekwa na serikali Bungeni, hupita pia TLS kwa ajili ya ushauri. Hata hivyo miaka ya karibuni inadhaniwa TLS kuingiliwa na siasa za vyama au harakati; mambo ambayo yanaweza kuzua hofu kwa watawala. Kwa hiyo ni wazi uchaguzi wa Rais wa TLS huangaliwa kwa jicho la tatu...!Kumradhi wanabodi kuuliza si ujinga naona tu nguvu nyingi sana zina tumika kuhakikisha TLS Inapata kiongozi fulani. Pengine tofauti na jumuiya zingine nyingi ambazo wahusika huchaguana tu na sa nyingine huchaguana kimyakimya lakini kwa TLS hali ni tofauti sana
Natamani sana kujua nini nguvu ya TLS kwa kiwango cha kuifanya uchaguzi wake uvutie watanzania kwa wingi namna hii!!
TLS ni chama cha mawakili na nchi inaendeshwa kwa kufuata sheria, unategemea CWT itayumbisha nchi? pia ili uwe mwanachama wa TLS lazima uwe na degree + uwe wakili tofauti na CWT, CCM n.kKumradhi wanabodi kuuliza si ujinga naona tu nguvu nyingi sana zina tumika kuhakikisha TLS Inapata kiongozi fulani. Pengine tofauti na jumuiya zingine nyingi ambazo wahusika huchaguana tu na sa nyingine huchaguana kimyakimya lakini kwa TLS hali ni tofauti sana
Natamani sana kujua nini nguvu ya TLS kwa kiwango cha kuifanya uchaguzi wake uvutie watanzania kwa wingi namna hii!!