Naona nikienda kuwa academician, nimechoka ajira kwenye private sector

Hapo mkataba miaka mitano baada ya hapo anarudi benchi kusugua matako ajira yake sio ya kudumu

Hapo hana cha mafao ya kustaafu

Amekalia kuti kavu mda wowote wanakuondoa inategemea mabosi wameamkaje

Huna uhuru
Uhuru maybe uko sawa… maana mostly masaa ya kazi yanaisha saa 11 jioni

Mafao yapo as usual, usiongee kitu usichokijua.

Mikopo ipo as usual…
 
Kimsingi that was my dream job ila sasa sikufanikiwa kuokota the required grades. Nilimiss 3.8 Gpa by a few points it hurt me alot sababu naelewa nilihujumiwa tu na uwezo ninao. Huwa nawaza sijui nifanye post graduate na masters niweze ingia huko ila nikiwaza competition ilivyo dah.
Ila walimu wa chuo wana enjoy sana muda wao hasa wanaoishi campus.
 
Aiseee 😃😃
Nimeshindwa hata kushangaa


Kipi exactly ambacho huenjoy hapo ulipo?? Masaa ya kazi ni mengi au? Au maboss kelele mingi?
 
Pole sana mkuu.
 
Labda kwa huo upande…

Maana huku siku boss akiambiwa amchomeke mtoto wa shangazi yake basi ni anasakwa mtu wa kunyofolewa 🙃
Hahahaaa....
Kwa sauti ya watangazaji wa mpira:

"Ananyanyuliwa kutoka benchi, ni mtoto wa shangazi huyu anapashapasha misuli hapa...."
"Hebu tuone nani atakwenda nje kutoa nafasi kwa kijana machachari kutoka ushangazini..."

Hapo akina Depal wanatetemeka kwa hofu huko ndani
 
Inasikitisha sana 😂


Muhimu ni mtu kuwa responsible for your duties, inakupunguzia chances za kukutana na misala ya dizaini hiyo..

Ila ukiwa wale file lako lina warning letters za hapa na pale, mara kuna tetesi unakulana na work mate, mara hauko neat and timely kwenye majukumu yako... wee hapo inakuwa ni one mistake kwako, one goal kwa mtoto wa shangazi 🥲
 
Hapo kwenye kukulana na work mate nadhani hakuna baya. Except "uingilie maeneo tengefu" (vya wakubwa wako).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…