Peter Mabala
JF-Expert Member
- Jul 19, 2016
- 1,216
- 1,685
Mzazi weka mchanganuo wa siku zilizopotea unaposema robo mwaka sikuelewi.Binti assume mtoto analipiwa 5,600,000/=,na robo mwaka mtoto amekaa nyumbani.So you want to tell me kwamba mzazi kwa masaa ya ziada mwalimu atakayofundisha mzazi alipe 1,400,000?That is too much,na sio halali.We know kuna masaa ya ziada,lakini tunataka kuwe na dialogue kati ya shule na wazazi,ili wakubaliane on logistics.Shule zisijiamulie zenyewe.
Timiza wajibu wako upatiwe haki yako.Naomba unielewe,watoto hawahamishwi,ila haki lazima itendeke.
Wajibu wa kuibiwa,wewe vipi?
Sijawahi ona mzazi ambae alishindwa kuwaelewa walimu. Hata wewe baada ya tarehe 28 utasahau kila kitu. Ugumu huwa upo mtoto kutoka nyumbani kwenda shuleni ila anapofanikiwa kutoka kila kitu hukaa sawa.Kwa hiyo unapindisha haki kwa vile tayari watoto wako enrolled kwako.Subiri mwakani.
Mar 17-June27>Miezi 3 na siku kadhaa nyumbani.Mzazi weka mchanganuo wa siku zilizopotea unaposema robo mwaka sikuelewi.
Zungumza fact zaidi ya siasa ili ushawishi wako uwe na uhalisia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kasema wasidaiwe kile kipindi walichokuwa likizoKasema busara itumike
Tazama upande wa pili pia walimu watakavyo wajibika bila mapumziko toka tarehe 29 june mpka tarehe 18 December. Miezi sita bila mapumziko.Ufafanuzi ni muhimu, wizara itoe ufafanuzi na maelekezo kwani wenye shule ni wafanya biashara, watakao umia ni wazazi sio wenye shule
Hatujawahi kuwa na situation kama ya mwaka huu mkuu,kwa hiyo usi generalize.Things might be extremely different.Sijawahi ona mzazi ambae alishindwa kuwaelewa walimu. Hata wewe baada ya tarehe 28 utasahau kila kitu. Ugumu huwa upo mtoto kutoka nyumbani kwenda shuleni ila anapofanikiwa kutoka kila kitu hukaa sawa.
Huo ndio uhalisia.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wasaidiwe?Wazazi hawataki kusaidiwa,wanataka haki!Kasema wasidaiwe kile kipindi walichokuwa likizo
Sio kwa kulipa ada yote kwa mwaka!Lakini kwa nini hamtaki kukaa na wazazi mkaongelea swala hili?Tazama upande wa pili pia walimu watakavyo wajibika bila mapumziko toka tarehe 29 june mpka tarehe 18 December. Miezi sita bila mapumziko.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa sasa nimekuelewa ila sahihi iko hivi.Mar 17-June27>Miezi 3 na siku kadhaa nyumbani.
Na ni bora shule zimefunguliwa zingeendelea kufungwa hali ingekuwa mbaya zaidi. Hapa serikali ipongezwe.Hatujawahi kuwa na situation kama ya mwaka huu mkuu,kwa hiyo usi generalize.Things might be extremely different.
Nimeweka ufafanuzi hapo juu kiongozi utakapoupitia[emoji116]Sio kwa kulipa ada yote kwa mwaka!Lakini kwa nini hamtaki kukaa na wazazi mkaongelea swala hili?
Ndalichako Hana kauli ya moja kwa moja kuhusu ulipaji wa ada kwa shule za binafsi. Kauli ya mwisho imeachwa kwa kamati na bodi za shule.Kwani Ndalichako amesemaje kwenye hili?
Vyote hata huduma nayo hua inahitaji mapato fulani ili kujiendeshaKwani shule za binafsi ni biashara au ni huduma?
no please mkataba haukuwa kufundishana mitandaoni!!! kuna chakula kinakuweko kwenye ada walikula mtaandaoni?kuna boarding cost walilala mtandaoni wa shule?nk
Naona leo mmetumia akili zenu kufikiri. Hili swala sisi wazazi tunaangalia serikali itasema nini. Maana kuna ada ya ufundishaji, chakula na usafiri kwa wale wa day. Hata kama walifundishwa mitandaoni lakini chakula hawakutumia cha Shule, wala hakukua na usafiri uliotumika.Gharama za bweni na usafir nazo zilitolewa kwa njia ya mtandao?
Acha kufananisha Ufundishaji na mambo yasiyoeleweka. Kwa hiyo unataka kusema Kama watoto wamekaa nyumbani miezi mitatu basi watasoma mpaka February ndio wamalize?Ndalichako Hana kauli ya moja kwa moja kuhusu ulipaji wa ada kwa shule za binafsi. Kauli ya mwisho imeachwa kwa kamati na bodi za shule.
Kufundisha mtoto ni sawa na kujenga nyumba. Anayejenga nyumba huanza kujenga mstari wa Kwanza, halafu mstari wa pili hujengwa juu ya mstari wa Kwanza. Hali kadhalika mstari wa tatu hujengwa juu ya mstari wa pili. Ikitokea siku ya kujengwa mstari wa pili kukatokea dharula na ujenzi usifanyike, bado dharula ikiisha mstari wa pili LAZIMA ujengwe kabla ya kujenga mstari wa tatu. Hakuna namna ya kujenga mstari wa tatu KABLA ya kujenga mstari wa pili.
Kwa hiyo mjenzi ni lazima aijenge nyumba ikamilike na LAZIMA alipwe malipo YOTE Kama walivyopatana awali.
Hali kadhalika, masomo na vipindi ambavyo watoto wangefundishwa mwezi wa nne na wa tano LAZIMA wafundishwe kabla ya kufundisha masomo na vipindi vilivyoko kwenye ratiba ya mwezi wa Saba. Ndiyo maana ni LAZIMA kutafuta nyongeza ya muda ili kufidia vipindi vilivyopotea wakati wa likizo ya dharula iliyotokana na mlipuko wa ugonjwa wa covid 19.
Kwa hiyo LAZIMA wazazi walipe ada ambayo hawakuilipa maana watoto wao LAZIMA wafundishwe na waalimu LAZIMA walipwe mishahara yao ambayo haikulipwa maana kazi wataifanya kikamilifu katika kuwafundisha watoto. Huo ndio utaratibu.
Sidhani Kama Kuna mzazi anategemea waalimu wataruka sehemu ya mada bila kuzifundisha kwa kuwa ilikuwa zifundishwe mwezi wa nne na wa tano.
Kwa mantiki hiyo haitegemewi mzazi kudhani kuwa hatadaiwa kulipa ada YOTE.